Kesi ya kumbaka mwanafunzi inayomkabili mwalimu wa Skuli ya Msingi Madungu Ali Makame Hatib 25, imeanzwa kusikilizwa ushahidi kwa mara ya kwanza juzi Septemba 05.09.2022, ambapo shahidi nambari moja ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano mwenye umri wa miaka 11 na mama yake mzazi wametoa ushahidi mbele ya hakimu wa Mahakama ya makosa ya udhalilishaji Muumini Ali Juma.
Ilielezwa Mahakamani hapo na Mwendesha mashtaka
wa Serikali Seif Mohammed Khamis, kwamba siku ya tarehe 12/08/2022 majira ya
saa 11:30 za jioni huko Skuli ya Msingi Madungu Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa
Kusini Pemba, Mshitakiwa ambaye ni Mwalimu wa Skuli ya Msingi Madungu Ali Makame
Hatib mwenye umri wa miaka 25, alimbaka mwanafunzi wa darasa la tano mwenye umri wa miaka kumi na
moja jina limehifadhiwa jambo ambalo ni kosa kisheria.
Ikumbukwe kuwa, kwa mara ya kwanza kesi hiyo ilitajwa Mahakamani Agosti 22.2022, ambapo mshitakiwa aliamuriwa kwenda
rumande hadi tarehe 05.09.2022 kwa ajili ya kusikilizwa kwa ushahidi.
Kesi hiyo imeghairishwa hadi tarehe 14.09.2022
ili kuendelea na ushahidi.