Kesi ya tuhuma za Ubakaji inayomkabili mwalimu wa Skuli ya msingi Madungu aliefahamikwa jina la Ali Makame Khatib mwenye umri wa miaka 25, mkaazi wa Matuleni Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, juzi 20.09.2022 imeendelea kwa kusikilizwa ushahidi kutoka kwa daktari aliyemfanyia vipimo msichana aliyefanyiwa vitendo vya udhalilishaji na mwalimu huyo mara baada ya msichana huyo kufikishwa hospitali ya Chake Chake kwa ajili ya uchunguzi.
Picha kutoka Maktaba
Akitoa
ushahidi mbele ya mahakama hiyo daktari huyo amesema kuwa vipimo vya awali
alivyofanyiwa mtoto huyo mara baada ya kuripotiwa kwa tuhuma za kufanyiwa
vitendo vya udhalilishaji vimeonesha kuwa mtoto huyo amefanyiwa vitendo vya
udhalilishaji.
“Mheshimiwa vipimo vya awali tulivyomfanyia
muathirika mara tu baada ya kufikishwa hospitalini vimeonesha kuwa tayari mtoto
huyo ameingiliwa katika sehemu zake za siri za mbele kwa mara kadhaa” alisema
daktari huyo
Ikumbukwe kuwa, kesi hiyo
iliripotiwa mahakamani hapo tarehe 05..2022, ambapo ilielezwa mahakamani hapo na
mwendesha mashtaka wa Serikali kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Seif
Mohammed Khamis, kuwa Agosti 12, 2022 majira ya saa 11:30 za jioni huko katika
skuli ya Msingi Madungu, Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, mshitakiwa
alimbaka msichana mwenye umri wa miaka 11 anaesoma darasa la tano ambapo ni
kosa kisheria.
Kesi
hiyo imeghairishwa tarehe 03.2022 itakapoendelea na ushahidi.