Familia moja katika kaunti ya Makueni nchini Kenya imelazimika kuahirisha hafla ya mazishi ya ndugu yao baada ya madai ya kutoweka kwa maiti.
Kulingana na familia ya Waema Nguku, 95, mwili waliopewa na Hospitali ya Rufaa ya Makueni, haukuwa wa ndugu yao.
Wanasema walikuwa tayari wamenunua jeneza la mzee huyo na kuelekea makafani Alhamisi, Septemba 15,2022 kuchukua mwili wake ambapo walitarajia maziko kufanyika Jumamosi, Septemba 17 lakini mambo yote yaliyeyuko..
Hata hivyo, kizaazaa kilizuka wakati mwili wa mzee huyo ulikosekana kwenye hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Rufaa ya Makueni.
Waliporejea Ijumaa kufuatilia suala hilo, mmoja wa viongozi wa hospitali hiyo aliwaomba kuchukuwa mwili mwingine ili wakafanye mazishi kwa niaba ya mzee wao.
"Baada ya kushindwa kutonyesha mwili wa baba yetu, tuliondoka na kurejea Ijumaa kufuatilia. Mmoja wa wasimamizi wa hospitali hiyo alituambia tuchukuwe mwili mwingine lakini tulikataa," alisema kifunga mimba wa mzee huyo, Kamene Waema.
Moja ya familia zilizozika jamaa wao wiki jana, imethibitisha kuwa ilipewa mwili usiokuwa sawa na kuutambua kama wa Mzee Nguku. Kufuatia ripoti hiyo, familia ya Nguku sasa inasubiri ripoti ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI) ili kwenda kufukua kaburi.
Msimamizi wa Hospitali ya Rufaa ya Makueni, Joseph Masila alisema suala hilo linachunguzwa kutambua ni familia ipi ilipewa mwili usio wao.
Rekodi za hospitali hiyo zinaonyesha kuwa miili 12 ilichukuliwa kwa mazishi wiki jana ambapo tano ilikuwa ya wanaume.
chanzo;The Standard