Wakizungumza na kipindi cha Mawio wananchi wa eneo hilo, wamesema wamechoshwa na tabia ya mama huyo ya kumgeuza kitega uchumi mtoto wake kwa kusingizia kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na wakaazi wa eneo hilo kitendo ambacho wamedai sio cha kweli na kinawaondoeshe heshima na uaminifu.
“Huyu mama ana tabia mbaya sana kila siku anadai mtoto wake amedhalilishwa sijui amebakwa sisi ndio wenyeji wa mtaa huu kwa muda mrefu na hatujawahi kusikia tabia kama hizo, lakini tangu alipokuja kuhamia yeye anasema mtoto wake anabakwa mtoto wenyewe mmoja kwahivyo tumechoshwa na tabia zake tuomba ahamishwe anatutia aibu na kutuvunjia heshima” alisema mama mmoja miongoni mwa wananchi hao.
Mmiliki wa nyumba ambayo amepanga mama huyo, amesema tayari ameshamrudishia fedha zake ambazo alilipia pango pamoja na kumpa siku tatu kuhama nyumbani kwake lakini amejiongezea siku tano za kuendelea kuishi katika nyumba hiyo, hivyo basi ameomba msaada kutoka mamlaka husika ili kumuhamisha mama huyo.
“Ninavyo zungumza hapa ana siku ya nane hajahama kwahivyo anaonesha ni jinsi gani mtu huyo ni mkorofi majirani wananisubiri mimi tu ni waruhusu ili waweze kumtoa” Alisema mmiliki huyo wa nyumba
Amani Ayoub Makame ni Sheha wa Shehia ya Mwanakwerekwe, amekiri uwepo wa tabia hiyo inayofanywa na mama huyo, nakusema amechukua hatua za kutoa taarifa kwenye kituo cha Polisi Kijito Upele na hatua za kumuhamisha ameshazifikisha kwa Mkuu wa Wilaya ya Mjini ili kufanyika kwa zoezi hilo.
Juhudi za mawio za kumtafuta mama huyo ili kutoa maelezo juu ya shutuma hizo ziligonga ukuta kutokana na kukataa kutoa ushirikiano.