Mkutano Mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi umemtimua uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, James Mbatia na kumvua Uongozi wa Makamo Mwenyekiti wa Chama hicho Angelina Rutairwa.
Aidha, Mkutano huo uliwataka viongozi wote wLiohusika na ubadhirifu wa Mali akiwemo Mbatia kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mkutano huo umefanyika Leo Jumamosi September 24, jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wajumbe 224 kati 368 waliopo Kwa mujibu wa Chama hicho.