Imeelezwa kuwa vitendo vya mauaji vinavyoendelea nchini hususan ni vya wanandoa vinasababishwa na wivu wa kimapenzi jambo ambalo inadaiwa ni kutokana na ukosefu wa elimu ya ndoa kabla ya wawili wapendanao kuishi pamoja.
Kutokana na wimbi hilo la mauaji, viongozi wa dini wanashauliwa kuendelea kutoa elimu ya ndoa kwa waumini wao kabla ya wawili wanaopendana kuingia kwenye ndoa hatua ambayo itasaidia kupunguza mauaji nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Shekh wa mkoa wa Mwanza, Shekh Hassan kabeke katika mkutano Viongozi wa dini, kamati ya kupinga na kutokomeza ukatili pamoja na Shirika la kutetea haki ya wasichana na wanawake la Kivulini waliokutana kujadili namna ya kutokomeza vitendo hivyo.