MKE AJINYONGA KISA KATUHUMIWA KUMUIBIA MUMEWE TSH 10,000/=

0

 Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Asia Kibishe (27) mkazi wa Kitongoji Cha Kazilamagembe kijiji cha Nyarututu kata ya Bwanga wilayani Geita amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga chanzo kikiwa ni kutuhumiwa kuiba Sh 10,000/=.


Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi (ACP) Henry Mwaibambe amesema tukio hilo lilitokea Septemba 1 2022 majira ya saa 7:30 asubuhi.

Kamanda Mwaibambe amesema marehemu alikutwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kipande cha kanga ambapo marehemu mwili wake ulikutwa umening’inia kwenye mti ulio karibu na nyumbani kwao.

“Chanzo cha tukio hilo ni mgogoro kati yake na mme wake aitwaye Fabian Shija (23), ambaye ni mkulima na mkazi wa kijiji hicho cha Nyarututu kwamba alikuwa anamtuhumu marehemu kumuibia Shilingi elfu kumi iliyokuwa chumbani kwao.” Amesema Mwaibambe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top