Mkutano wa nane wa baraza la kumi na wawakilishi unatarajiwa kuanza leo katika ukumbi wa baraza hilo Chukwani.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari katibu wa
baraza hilo Bi. Raya Issa Msellem, amesema miongoni mwa shughuli
zitakazofanyika katika kikao hicho ni
kujadili wa mswada wa Sheria ya kufuta Sheria namabri 4 ya mwaka 2007 ya baraza
la Wawakilishi kuhusiana na kinga, uwezo wa fursa katika utekelezaji wa kazi na
mswada wa Sheria ya kuanzishwa kwa taasisi ya wahasibu, wakaguzi na washauri
elekezi wa kodi Zanzibar.
Aidha kikao hicho, kitapokea kauli ya Serikali
kuhusiana na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kupatiwa majibu
maswali 159 yatakayowasilishwa na wajumbe pamoja na kupokea taarifa ya Serikali
kuhusiana mchezo wa ngumi Zanzibar.
Hivyo basi, Bi. Raya amewaomba wananchi kufatilia
kwa karibu yatakayoendelea katika mkutano huo ili kutambua mambo mbali mbali yenye
maslahi ya nchi.