MAMA MBARONI KWA KUMUUA MTOTO WA MCHEPUKO WA MUMEWE KISHA KUMZIKA POLINI

0

 Jeshi la polisi mkoa wa Njombe linamshikilia Happines Mkolwe[27] mkazi wa kijiji cha Ihanga halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Jackson Kihungo mwenye umri wa miaka 6 wa mama aliyekuwa na mahusiano na mumewe.


Mbele ya vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema mtuhumiwa huyo baada ya mahojiano amekiri kutekeleza mauaji hayo baada ya mumewe ambaye waliachana kudaiwa kuwa na mwanamke mwingine.


*UJUMBE WA LEO*

Woga nao unawarudishaga sana nyuma watu,ukiogopa sana hasara huji kufanya biashara yoyote duniani hapa utakuwa unaishia kutunza hela ndani zisizoongezeka


Karibuni Wana Kalynda tuwaoneshe watu Uzuri wa Kalynda,kwani kampuni hii ni tofauti na kampuni zingine,hii inafanya kazi Kwa mujibu wa sheria kama una wasiwasi fuatilia kila siku saa mbili asubuhi ITV uone kazi zao.

🔴WOGA WAKO NDIO UMASIKINI WAKO!
Wivu wa mapenzi ndio unaotajwa kusababisha ukatili huo uliosababisha mauaji ya mtoto huyo wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Ihanga ambapo Happiness alimchukua mtoto huyo wakati akitoka saluni kunyoa na kwenda naye polini wanakopasulia mbao na kisha kumuuwa na kumfukia kwenye masalia ya mbao.

Sanjari na tukio hilo lakini pia Kamanda Issa amewataka wananchi wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzirejesha kwenye mamlaka zinazohusika katika kipindi hiki cha mwezi septemba kabla msako mkali haujaanza.

Baadhi ya wakazi wa Njombe akiwemo Lukule Mponji wamesema vijana ndio wamekuwa na tabia ya kujihusisha kimapenzi bila utaratubu mzuri na ndio chanzo kinachosababisha mauaji hayo.

Juu ya usalimishaji wa silaha wanasema hatua hiyo ya jeshi la polisi ina dhamira njema kwani itasaidia sana kupunguza vitendo vya kihalifu vinavyofanywa kwa kutumia silaha hizo huko uraiani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top