MWANAFUNZI AUA BAADA YA KUSHINDWA KUBAKA

0

 

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Sinde jijini Mbeya, Faraja Kasole (16), ameuawa kwa kukatwa na shoka shingoni na mwanafunzi mwenzie aitwaye Humphrey Ngogo (17) mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya sekondari Iduda, baada ya kushindwa kumbaka.

Chanzo cha mauaji hayo kimedaiwa kuwa ni tamaa za kimwili ambapo mtuhumiwa Ngogo alifanya jaribio la kumbaka marehemu, lakini baada ya kuzidiwa nguvu akachukua shoka na kumpiga nalo kichwani.

Kamanda wa Jeshi la Polisi, mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa alifika nyumbani kwa marehemu ambaye kwa muda huo alikuwa peke yake na kisha kumvamia chumbani kwake kwa nia ya kumbaka na alipozidiwa nguvu ndipo aliamua kuchukua shoka na kumpiga nalo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mjomba wa marehemu Faraja Kasole, aitwaye, Sauli Mwaisenye, amesema maziko yalifanyika Septemba 4 mwaka huu katika makaburi ya Iyela jijini Mbeya, na kwamba familia inaomba vyombo vya maamuzi kutenda haki.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top