Mwanamke mmoja ameshindwa kuzuia hasira zake baada ya kudai kupigwa ngumi ya usoni na mchungaji wakati akimuombea.
Katika video iliyopostiwa kwenye Mtandao wa TikTok, mwanamke huyo anaonekana akiongea kwa hasira kwamba mchungaji alikuwa akimuombea na kumpiga ngumi kwa uchungu usoni kama njia ya kumsukuma kuanguka chini ili kudhihirisha kwamba ameingiwa na Roho Mtakatifu.
Mwanamke huyo anaeleza kwamba imekuwa mazoea ya mchungaji huyo kumpiga kwa ngumi mpaka macho yake mara nyingine yanapata uvimbe kutokana na maumivu ya ngumi za mchungaji.
Mwanamke huyo anasema mchungaji huwa anapiga watu ngumi usoni kama njia ya kuyaondoa mapepo ndani mwao na kuwatakasa.
“Mchungaji alikuwa anataka kunifanyia utakaso, ananipiga ngumi machoni mpaka macho yangu yanavimba," mwanamke huyo anaeleza.
Video hiyo imeibua maoni tofauti ambapo wengine wanamhurumia na wengine wanamtania kuwa huwenda hatoi sadaka kanisani.
Wengine waliendeleza utani kwamba hilo ni onyo dhidi ya watu wanaofikiria kwenda kanisani na kufuata kila agizo la mchungaji mpaka lile la kupotosha eti kwa sababu ni mtu wa Mungu.
Credits: globalpublisher