Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, imeshtushwa kiwango kikubwa cha kuvunjika kwa ndoa nchini chanzo kikubwa kikitajwa ni kumomonyoka kwa maadili huku Dar- Es- Salaam ikitajwa kuwa ni Mkoa ambao unaongoza idadi ya ndoa nyingi kuvunjika ambapo takriban ndoa 300 huvunjika kila mwezi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti na
kamati hiyo, Stanslaus Nyongo, baada ya kukutana na Wizara ya Maendeleo ya
jamii, jinsia na makundi maalum.
“Tumepata hesabu ya ndoa kuvunjika
kwa mfano Dar- Es- Salaam pekee yake zaidi ya ndoa 300 kwa mwezi zinavunjika. Hili
tunaona ni tatizo kubwa ni janga, sisi kama kamati tunaona haja kubwa ya
kuishauri Seerikali kuona jinsi gani ya kuchukua hatua kwa ajili ya kupambana
na hali ii iliyopo” amesema
“Hili limeshamiri sana katika jamii
yetu, na kwakweli kuna haja ya Serikali kutafuta kwa kina chanzo nini kuona ni
hatua gani za kuchukua” amesema
Chanzo. Mwananchi Official