Jumuiya ya Mazingira na Utetezi wa Kijinsia Kisiwani Pemba ‘PEGAO’ imepokea ripoti ya miezi mitatu kutoka mwezi April hadi June kutoka kwa wahamasishaji jamii kuhusu mradi wa kuwahamasisha wanawake kugombea nafasi mbali mbali za uongozi pamoja uimarishaji wa demokrasia nchini.
Akipokea ripoti hiyo, Mkurugenzi kutoka jumuiya ya Mazingira na Utetezi wa Kijinsia Pemba ‘PEGAO’ Hafidh Abdi, amewaomba wahamasishaji jamii hao kuongeza juhudi katika kuwafikia wananchi pamoja na kufahamu lengo mahsusi la mradi huo ili liweze kufikiwa ipaswavyo.
“Kwanza munatakiwa muwe na juhudi
binafsi katika jambo hili ili kuwafikia wananchi wengi ziadi hususan akina mama
ambao ndio tunawalenga zaidi lakini kufahamu lengo letu ni lipi haswa ili
tunapokutana na wananchi licha ya kusikiliza changamoto zao tuweze kufanikisha
lengo la mradi huu ambalo ni kuwahamasisha akina mama kugombea nafasi mbali
mbali za uongozi pamoja na uimarishaji wa demokrasia katika vyama vya Siasa”
alisema
Akiwasilisha ripoti hiyo ya mwezi
April hadi June, muhamasishaji jamii kutoka Wilaya ya Wete Raya Said Ali,
amesema katika Shehia ya Mjananza wananchi wanakabiliwa na changamoto mbali
mbali ikiwemo akina kutokujua kusoma na kuandika, ukosefu wa Kituo cha Afya, ukoseu
wa maji safi na salama, utoro kwa wanafunzi na kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa pamoja
na vyeti vya vifo.
Ameongoza kuwa, licha ya changamoto
hizo asilimia 90 ya akina mama wamekubali kugombea katika nafasi mbali mbali za
uongozi na kuomba kupatiwa elimu ili wawe na uwezo wa kugombania nafasi hizo
ipaswavyo.
“Kwakweli wana shehia ya Mjananza
licha ya changamoto zote walizonazo ikiwemo changamoto ya kutokujua kusoma na
kuandika lakini wote wamekubali kugombania nafasi mbali mbali za uongozi” Raya
Said Ali
Siti Habib Mohammed ni Muhamasihaji jamii
Wilaya ya Mkoani, akiwasilisha ripoti hiyo, amesema katika Shule ya Kunguni
Wambaa inakabiliwa na uhaba wa walimu jambo ambalo linapelekea wanafunzi
kutokufika Shuleni kwa wakati sambamba na kutoroka pamoja na kukosa masoma ya
uhakika kwa wanafunzi ambao wanasilia shuleni hapo.
“Skuli ina marada 13 kuanzia
maandalizi hadi darasa la saba, ambapo skuli mzima ina walimu wanawake watatu
na walimu wakiume wawili huku wanafunzi 682 ambapo kila mwalimu analazimika
kufundisha wastani wa wanafunzi 136 katika mazingira hayo elimu bora itapatikana
vipi” alihoji
Katika hali isiyo ya kawaida
muhamasishaji jamii huyo, amesema katika changamoto nyengine walioibua ni uwepo
wa familia ambayo ina watoto watano wenye ulemavu wa viungo katika Kijiji cha
Kwa-Azani, ambapo Mama wa familia hiyo amesema anatamani kugombea nafasi mbali
mbali za uongozi lakini kutokana na changamoto ya ulezi wa watoto wake wenye
ulemavu ndio chanzo cha yeye kushindwa kugombea nafasi za uongozi katika jamii
vyama vya siasa.
“Kwahivyo katika harakati zetu za
kuendelea kuihamasisha jamii tulikutana na huyo mama mwenye watoto watano ambao
wote wana ulemavu wa viungo, tulipomtaka agombee nafasi mbali mbali za uongozi
amesema hawezi kugombea nafasi za uongozi kutokana na hali ya watoto wake kuwa
walemavu na kushindwa kupatiwa msaada wowote kutoka Serikalini wala taasisi
binafsi kibaya zaidi imewabidi kukatisha masomo” alisema
Amesema, Changamoto nyengine zinazowakabili wananchi wa shehia hiyo ni ubovu wa barabara kutoka Kijiji cha Wambaa hadi Kijiji cha Kutukuu changamoto ambayo inapelekea wananchi wa maeneo hayo kushindwa kufanya shughuli zao za maendeleo ipaswavyo.
Muhamasishaji jamii kutoka Wilaya ya Mkoani Siti Habib Mohammed, akiwasilisha ripoti kuhusu changamoto zinazowakabili wananchi wa Shehia ya Wambaa.
Nae, muhamasishaji jamii kutoka
Wilaya ya Michewezi Asha Rashid Abdalla, amesema wananchi wa Shehia ya Kinowe
wanakabiliwa na Changamoto ya miundo mbinu bora ya barabara hususah kipindi cha
msimu w mvua jambo ambalo linapelekea kudumaa kwa shughuli zinazowaingizia
wananchi kipato.
Aidha, amesema miongoni mwa
changamoto zinazowakabili wananchi hao ni ukosefu wa huduma ya nishati ya umeme
pamoja na utoro wa wanafunzi mashule hali inayopelekea kuongezeka kwa vitendo
viovu mitaani ikiwemo utumiaji wa dawa za kulevya, wizi na vitendo vya
udhalilishaji.
Aidha, amesema changamoto nyengine zinazowakabili wananchi hao ni uwepo wav yeti feki vya kuzaliwa, uchache wa fursa za ajira, hali ngumu ya maisha pamoja uchache wa madara na waalimu katika skuli ya Msingi ya Chimba idadi ya madarasa 17, wanafunzi 1024 na walimu 17.
Muhamasishaji jamii kutoka Wilaya ya Michewezi Asha Rashid Abdalla, akiwasilisha ripoti kuhusu changamoto zinazowakabili wananchi wa Shehia ya Kinowe na Chimba, zinazopelekea Akina mama kushindwa kugombea nafasi mbali mbali za uongozi katika vyama vya siasa.
Hasina Omar Salim, ni muhamasihaji
jamii kutoka Wilaya ya Chake Chake, amesema
changamoto inayowakabili wa Shehia ya Wara ni maelewano madogo baina ya
wananchi wa Kijiji cha Mbuni na Mamlaka ya Maji Zanzibar ‘ZAWA’ changamoto
ambayo ametokana na wanakijiji kuona kuwa sio haki kulipia bili ya maji kwa
mamlaka hiyo, kwani huduma hiyo wamepatiwa na mfadhili ambaye ni tofauti na
mamlaka hiyo.
Akitaja changamoto nyengine, amesema kuporomoka kwa maadili, utumiaji wa dawa za kulevya, unyanyasaji wa kijinsia pamoja na wizi ambao unahusisha vijiji vya Makondeko, Kiumbe Mzito na Ujinga hali ambayo inasababishwa na kukosekana kwa mashirikiano kati ya wanajamii na vyombo vya usalama.
Amesema Changamoto nyengine zinazowakabili wananchi hao ni ubovu wa miundombinu ya barabara za ndani hususan katika Kijiji cha Shimoni, hali inayopelekea changamoto kwa wafanyabiashara kutokufika sokoni bidhaa zao kwa wakati.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi huo kutoka ‘PEGAO’ Dina Juma Makota, amewasihi wahawasishaji jamii hao kufuata sheria na kanuni katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuepuakana usumbufu unaoweza kutokeza sambamba na kuzingatia malengo ya mradi huo ambayo ni kuwahamasisha akina mama katika kugomania nafasi mbali mbali za uongozi pamoja uimarishaji wa demokrasia katika vyama vya siasa.