SISI SOTE NI WALEMAVU WATARAJIWA HATUNA BUDI KUWAJALI WENYE ULEMAVU LEO- DC MJAJA.

Hassan Msellem
0Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mheshimiwa Khatib Juma Mjaja, ameziomba taasisi mbali mbali Kujitokeza katika kuwasaidia watu wenye ulemavu nchini ili nao waweze kuishi maisha mazuri yenye furaha na Amani kama wanavyoishi wengine.


Mkuu huyo, ametoa kauli hiyo katika hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali Kwa watu wenye ulemavu huko katika Skuli Sekondari Michenzani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, amesema jukumu la kuwasaidia watu wenye ulemavu sio jukumu la Serikali pekee, hivyo basi mashirka na taasisi binafsi zinapaswa kutoa misaada mbali mbali kwa Watu wenye Ulemavu kwani Kila mtu ni mlemavu mtarajiwa.


"Suala la kuwasaidia watu wenye ulemavu sio suala la Serikali pekee Bali hata mtu mmoja mmoja mwenye uwezo, mashirika na taasisi binafsi zinapaswa kuwasaidia kwani sisi sote ni walemavu watarajiwa kwani hata Hawa ambao ni walemavu Leo baadhi Yao walikuwa kama sisi" Dc Mjaja


Sambamba na hafla hiyo, Mheshimiwa Mkuu Wilaya, aliwatembelea watu wenye ulemavu na maradhi mbali mbali katika Shehia ya hiyo pamoja na kuwapatia misaada ya Sabuni na Pempasi ili kuwafariji kutokana na hali zao.

Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, akikabidhi msaada w bunda la Pempasi na Sabuni Kwa Kijana mwenye ulemavu wa viungo huko Tovukuu Michenzani.Kwa upande wake, Afisa wa watu wenye ulemavu Wilaya ya Mkoani Warda Waly Mohammed, amesema taasisi ya Anour Foundation kwa kushikiriana jumuiya ya  Vichwa vikubwa pamoja na Mkurugenzi wa Bandari Pemba, wameona kuna haja kubwa ya kuwasaidia watu wenye ulemavu Kisiwani Pemba ili nao waweze kujikimu kimaisha sambamba na kuondokana na changamoto mbali mbali.


Aidha Bi. Warda, amewaomba wazazi wenye watoto walemavu kutokuwafungia ndani na badala yake kuwatoa nje na kuwachanya na watu wasio na ulemavu ili waweze kupata haki zao za msingi ikiwemo kutambuliwa pamoja kujifunza mambo mbali mbali.


"Naomba niwasihi wazee wangu tusiwafungie ndani watoto wenye ulemavu Kwa kuhisi kuwa ukiwa na Mtoto mwenye ulemavu ni mkosi Bali kuwa ni Mtoto mwenye ulemavu ni jambo la kawaida kwani hakuna ambaye anapenda kuwa na mtoto mwenye ulemavu Bali ni mapenzi ya mungu" Bi. Warda

Afisa watu wenye ulemavu Wilaya ya Mkoani Wadra Waly Mohammed, akizungumza na wananchi pamoja na watu wenye ulemavu katika Skuli ya Sekondari Michenzani.


Miongoni mwa watu wenye ulemavu waliopatiwa msaada katika hafla hiyo ni Fatma Silima Ali, ambaye alipatiwa msaada wa Pempasi na Sabuni, Khadija Ali Hassan, ambaye alipatiwa msaada kiti mwendo na Pate Makame Amani, ambaye alipatiwa msaada wa Sabuni.


Nae, mwanafunzi anayesoma kidato kwanza anayesoma Skuli ya Sekondari Michenzani Abdallah  Mohammed makame, ameiomba msaada wa kifaa vya kutembelea (White Cane) kifaa cha kurekodia sauti, karatasi ya A4 frame Kwa ajilia ya kuandika maandishi ya Nukta nundu, Mwalimu wa Elimu mjumuishi (inclusive teacher) kifaa cha kuandia ili aweze kusoma katika mazingira rafiki kama wanafunzi wengine kwani kwasasa anasoma Kwa kusikiliza pekee na kufanya mitihani kwa njia ya mahojiano (interview).

Kati kati ni mwanafunzi Abdalla, aliyeomba msaada vifaa vya kusomea.Misaada hiyo, imejumisha viti mwendo vitano (5) vilivyotolewa na Zanzibar Anour Foundation, Sabuni Michi 35, iliyotolewa na jumuiya ya Vichwa vikubwa na mgongo wazi na Pempasi mabunda 35 yaliyotolewa na mkurugernzi wa bandari Kisiwani Pemba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top