TAASISI YA THE FUTURE LIFE FOUNDATION YATOA MSAADA WA MCHELE KWA WATOTO YATIMA 320 KISIWANI PEMBA.

Hassan Msellem
0

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mheshimiwa Abdalla Rashid Ali, ameipongeza jumuiya ya The Future Life Foundation Kisiwani Pemba kwa juhudi zake za kuwasiadia watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo watoto yatima, wajane na watu wenye ulemavu ili kuhakikisha kuwa nao wanaishi maisha ya amani na faraja.

Akimuwakilisha Mkuu wa MKoa wa Kusini Pemba Mhsehimiwa Matar Zahor Massoud, huko katika ukumbi wa Judo Gombani katika hafla ya kutoa msaada ya mchele kwa watoto yatima 320 kutoka maeneo mbali mbali Kisiwani Pemba, Mkuuwa Wilaya ya Chake Chake Mheshimiwa Abdalla Rashid Ali, amesema suala la kuwasaidia watu wenye mahitaji ni suala la muhimu katika maisha ya mwanadamu kwani hakuna mtu anaweza kujua kesho yake na familia yake hivyo basi kuwasaidia wengine ni miongoni mwa uwekezaji nzuri wa duniani na akhera.

 

“Sisi sote ni mayatima, wajane na walemavu watarajiwa hivyo basi hatunabudi kuwasaidia wenzetu ambao leo wanapitia katika hali hizo kwani hakuna mwenye uhakika wa kuijua kesho yake yeye na familia yake, kwahivyo unapowasaidia watu leo basi unaweza katika dunia yako na akhera yako” Mhe. Abdalla Rashid Ali

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mhe. Abdalla Rashid Ali, akizungumza na wananchi walioshiriki katika hafla ya utolewaji wa msaada wa Mchele katika Ukumbi wa Judo Gombani.

Kwa upande wake, rais wa taasisi ya The Future Life Foundation Sheikh Mborouk Seif Salim, amesema taasisi ya The Future Life Foundation imedhamiria kuwasaidia wananchi wanaokabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo watu wenye ulemavu, wajane, watoto yatima pamoja na wale wanaosumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu ili kuwapatia unafuu juu ya changamoto hizo zinazowakabili.


Ameongeza kuwa, taasisi hiyo inashirikiana na taasisi mbali mbali pamoja na wanajamii katika kuwakinga watoto dhidi ya janga la udhalilishaji linaloikabili Visiwa vya Zanzibar ikiwemo kuhakikisha wanaishi katika mazingira bora na salama.

Rais wa taasisi ya The Future Life Foundation Sheikh Mbarouk Seif Salim.

Akiwasilisha maombi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Sheikh Mborouk amemuomba mkuu huyo Wilaya kufikisha maombi ya kupatiwa huduma ya nishati ya Umeme na maji katika mradi wa viungo unaoendelea huko Kangagani ili kuondokana na ukosefu wa maji unaowakabili.


“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya The Future Life Foundation imeamua kujikita katika mradi wa viungo wenye thamani ya shilingi milioni 45 Zakitanzania lakini changamoto kubwa inayotukabili ni ukosefu wa maji na hiyo imetokana na ukosefu wa huduma ya Umeme, kiasi kwamba inatulazimu kwa siku kutumia shilingi elfu thelathini kwa ajili ya huduma ya umwagiliaji kiasi cha fedha ambacho ni kikubwa sana kwetu” Alisema


Aidha mkuu huyo, ameomba Serikali na wahisani mbali mbali kuinga mkono taasisi hiyo ili kuongeza uwezo wa kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo mayatima, wajane na watu wenye ulemavu.


Nae Sheikh Abdalla Mohammed Abdalla kutoka afisi ya mufti Pemba, amesema afisi ya Mufti Kisiwani Pemba imeamua kuwa bega kwa began a taasisi ya The Future Life Foundation katika juhudi wanazozifanya katika kuwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu ili kuhakikisha wanaondokana na mazingira hayo.

 

“Ndugu zangu ukweli kwamba katika jamii zetu zinazotuzunguka kuna watu wanakabiliwa mazingira magumu mno ikiwemo hawa watoto yatima, wajane na wale wanaosibiwa na maradhi mbali mbali hivyo basi katika kulitambua hilo ofisi ya mufti kisiwani Pemba kwa moyo wa dhati kabisa imeamua kwa hiari kushirikiana na taasisi hii katika kuendeleza jitihada za kuwasaidia watu wanaokabiliwa na shida mbali mbali” Sheikh Abdalla

 

Sheikh Abdalla, aliendelea kwa kutoa wito kwa watu wenye uwezo, mashirika pamoja taasisi mbali mbali katika kuwasaidia watu wanaokabiliwa na shida mbali mbali ili vipato vyao viweze kuwa msaada kwa wengine na viweze kubarikiwa.

Sheikh Abdalla Mohammed Abdalla kutoka afisi ya mufti Pemba.

Ali Msanif ni msimamizi wa shamba la mradi wa viungo unaoendeshwa na taasisi ya The Future Life Foundation Kangagani, amesema wananchi wa Kangagani wameamua kujiingiza vilivyo katika ujasiriamali wa kilimo cha mboga mboga na viungo lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji ya kumwagilia vipando vyao changamoto inayosababishwa na ukosefu wa nishati ya Umeme.

Ali Msanif ni msimamizi wa shamba la mradi wa viungo unaoendeshwa na taasisi ya The Future Life Foundation Kangagani.

Mariam Mohammed Muhene, ni miongoni mwananchi walipatiwa msaada huo wa mchele ameishukuru taasisi ya The Future Life Foundation kwa kuwajali watu wenye watoto yatima na kuziomba taasisi na watu wenye uwezo wa kifedha kujitokeza katika kuwasaidia watu wanye shida mbali mbali.


Mariam Mohammed Muhene, ni miongoni Mwa wananchi waliopatiwa msaada huo wa Mchele akitoa neno la shukurani kwa taasisi ya The Future Life Foundation.

“Kwakweli tumefarijika sana kupatiwa msaada huu kwasababu kama tuanvyojua kuwa sasa hivi hali ya maisha ni ngumu sana kwahivyo kutokea taasisi kama hii kutusaidia kilo tano za mchele ni jambo la kushukuru mno na sio kilo tano tu hata ingikuwa kilo moja tungalishukuru sana kutokana hali ilivyo kwahivyo nitoe wito kwa watu binafsi na taasisi mbali mbali wenye uwezo wajitoe katika kuwasaidia watu wenye shida mbali mbali ikiwemo watoto yatima wajane na wenye maradhi mbali mbali” Bi. Mariam Mohammed Muhene

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mhe. Abdalla Rashid Ali, akikabidhi msaada wa mchele kwa watoto yatima.

Msaada huo wa kilo tano (5) za Mchele umetolewa na taasisi ya The Future Life Foundation chini ya ufadhili wa kutoka nchini Canada, Ufaransa pamoja na Ubelgiji.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top