UMMY MWALIMU- BIMA HII NI KUPUNGUZA MZIGO WA GHARAMA ZA MAATIBABU

0

 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kufungamanisha umiliki wa kadi ya Bima ya Afya na upatikanaji wa huduma zilivyofungamanishwa na umiliki wa kadi au namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA).

“Kufungamanishwa kwa baadhi ya huduma za kijamii kunatarajia kuweka msukumo kwa Wananchi ili wachukue hatua za kujiunga na Bima ya Afya ili kuepuka changamoto ya kutopata huduma za afya bila kikwazo cha fedha”- Waziri Ummy Mwalimu

“Malipo ya Bima yanaweza kuwekewa utaratibu wa kulipwa kwa awamu kulingana na uhitaji wa Wateja na watoa huduma, Bima ya Afya kwa wote ni muhimu, ni bora kuchangia kidogo uwe na Bima ya Afya kuliko kusubiri ukiugua ukalipa fedha nyingi ili kupata matibabu”- Waziri Ummy Mwalimu

“Kwa wasio na uwezo Serikali itatumia utaratibu wa TASAF kuwatambua kwa ajili ya kuwapa huduma, Wananchi hawatalazimishwa kujiunga na mfuko mmoja, watakua wa na uhuru wa kuchagua skimu za Bima zilizosajiliwa kwa mujibu wa sheria, tutaweka utaratibu wa kuchangia kwa kuzingatia kaya, na Mtu mmoja mmoja asiye katika kaya”- Waziri Ummy Mwalimu

“Bima ya Afya kwa wote itakuwa na kitita cha msingi na vifurushi mbalimbali vitakavyowezesha wananchi kuchagua kulingana na mahitaji, hakuna atakayepigwa faini, atakayefungwa au kubughuziwa kwa namna yoyote ile kisa hatakua na Bima ya Afya, Bima ya Afya ni hiari, tutaendelea kuelimisha kuwa lengo la Serikali kupitia Bima hii ni kupunguza mzigo wa gharama za matibabu kwa Wananchi”- Waziri Ummy Mwalimu

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top