WAFANYA BIASHARA KISIWANI PEMBA WAOMBWA KUITUMIA 'ZFCT' KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO ZA KIBIASHARA.

Hassan Msellem
0

WAFANYA BIASHARA KISIWANI PEMBA WAOMBWA KUITUMIA 'ZFCT' KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO ZA KIBIASHARA.



Wafanya biashara kisiwani Pemba wameombwa kulitumia baraza la ushindani halali wa biashara katika kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili ikiwemo mfumuko wa bei.


Mapema akizungumza na wafanya biashara pamoja na wadau wa biashara huko katika ukumbu wa mikutano wa Hoteli ya Mkoani Pemba, mrajis wa baraza la ushindani halali wa biashara Fatma Gharib Haji, amesema lengo la kuanzishwa kwa baraza halali la ushindani wa biashara Zanzibar ni kutoa fursa kwa wafanya biashara na wateja kutoa malalamiko yao pamoja na maoni juu ya mustakabli wa mwenendo wa biashara visiwani Zanzibar.


Ameongeza kuwa, miongoni mwa majukumu ya chombo hicho ni kusikiliza rufaa zinazotokana na mamlaka na taasisi mbali mbali za udhibiti wa biashara ili kuhakikisha wafanya biashara pamoja na watumiaji wanapata haki zao za msingi ikiwemo kusikiliza rufaa zao na kuzipatia ufumbuzi.


“Baraza halali la ushindani wa biashara ni chombo ambacho kazi yake ya msingi ni kusikiliza rufaa zinazotokatana na na mamlaka na taasisi za udhibiti kama vile ZFCT, ZURA, mamlaka za usafiri wa anga na baharini, ZPRA, ZBS pamoja na ZFPA” Alisema


“Chombo hiki kipo kuweza kuwapa fursa watumiaji pamoja na wafanya biashara pale ambapo wamekwazika na maamuzi ambayo yametolewa na vyombo ambavyo nimevitaja hapo juu kuweza kukata rufaa kwa kupeleka malalamiko yao katika baraza la ushindani halali wa biashara” Mrajis ZFCT

Mrajis wa 'ZFCT' Fatma Gharib Haji, akitoa elimu kwa wafanya biashara juu suala la ukataji wa rufaa.


Kwa upande wake, kaimu mkurugenzi wa idara ya mashauri ZFCT Abass Juma Fakih, amewaomba wafanya biashara hao kuwa na ushindani halali wa biashara ili kulinda maslahi ya watumiaji wa biashara zao.


“Kuanzishwa kwa baraza hili ni kusimamia mambo mawili makuu ushindani halali wa biashara na kumlinda mtumiaji, kama kuna ushindani halali wa biashara bila ya shaka kutakuwa na ushindani kharamu wa biashara na mtumiaji ni lazima alindwe asipolindwa mtumiaji ataarhirika” alisema

Kaimu mkurugenzi wa idara ya mashauri ZFCT, Abass Juma Fakih, akitoa ufafanuzi juu ya ukataji wa rufaa Kwa wafanya biashara.


Akiwasilisha mada juu ya muongozo wa kukata rufaa kwa wfanya biashara, afisa uchumi kutoka baraza la ushindani halali wa biashara Zanzibar, Rabia Abdalla Said, amesema mrufani atawasilisha nakala nane za indhari ya rufaa katika baraza hilo ndani ya muda wa siku 30 tangu tume au mamlaka husika ya udhibiti ilipotoa uamuzi dhidi yake.


Wafanya biashara pamoja na wadau wa biashara wakiorodhesha dondoo muhimu katika mkutano huo.


Nae, mkurugernzi wa jumuiya ya wasaidizi wa Sheria Chake Chake Nassor Bilal Ali, ameuomba uongozi wa baraza hilo kuwa na ofisi Kisiwani Pemba ili wafanya biashara na watumiaji waweze kuwa na sehemu rafiki ya kupata huduma kwa haraka.


“Mara nyingi tumezoea kuona taasisi nyingi za Serikali kuwa na makao makuu yake upande wa kisiwa cha Unguja pakee na badala yake tunasikia Pemba kunakuwa na ofisi ndogo, kwahivyo naomba kama hamuna ofisi Pemba mufanye mpango iwepo ili wafanya biashara na wadau wenu waweze kupata huduma zenu kwa haraka” Mkurugenzi Chapo.



Mkurugenzi wa jumuiya ya wasaidizi wa Sheria Chake Chake Nassor Bilal Ali, akitoa ombi Kwa baraza la ushindani halali wa biashara Zanzibar.


Akitoa ufafanuzi kuhusu ombi hilo, mrajis wa baraza la ushindani halali wa biashara Fatma Gharib Haji, ameahidi kuliwasilisha ombi hilo kwa Mheshimiwa wa Waziri wa biashra na Viwanda ili kuona suala hilo linafanyiwa kazi.


Nassor Hakim Haji, ni MkurugenZi wa jumuiya ya wasidizi wa Sheria Wilaya ya Mkoani, amependekeza rufaa zinazokatwa kutokupelekwa mahakama ya rufaa ili kupunguza asumbufu kwa wafanya biashara pamoja na watumiaji.


Nassor Hakim Haji, ni MkurugenZi wa jumuiya ya wasidizi wa Sheria Wilaya ya Mkoani, akitoa pendekezo juu ukataji wa rufaa.


Akitoa ufafanuzi kuhusu pendekezo hilo, mrajis wa baraza hilo Fatma Gharib Haji, amesema kwa mujibu wa Sheria kesi zote ambazo zimehukumiwa na mahakamu kuu zinapaswa kusikilizwa na mahakama ya rufaa licha ya kukiri kuwepo kwa mapungufu ya kisheria na badala yake baraza hilo liweze kutoa maamuzi ya mwisho dhidi ya rufaa hizo.


Baadhi ya wadau walioshiriki katika mkutano huo wakifuatilia Mada.


Baraza la ushindani wa biashara lilianzishwa chini ya kifungu 26 cha Sheria ya ushindani halali wa biashara na kumlinda mtumiaji, Sheria nambari 5 ya mwaka 2018, na kuanza kazi zake rasmi mwezi Oktoba 2020 baada ya kukamilika kwa Mwenyekiti, Mrajis na Wajumbe wa baraza hilo.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top