Watumiaji wa KISIMBUZI cha Uunganishaji na Urushaji wa Maudhui Zanzibar ‘ZMUX’ katika kijiji cha Wambaa Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, amelalamikia ukosefu wa huduma za uhakika kutoka kwa kampuni hiyo kwa kipindi cha muda mrefu, jambo ambali linapelekea kutokufikia malengo ya kununua Kisimbuzi hicho.
Wakizungumza na idawaonline.com
baadhi ya wateja hao, wamesema tangu wanunue kisimbuzi hicho hawajawahi kupata
huduma kwa uhakika kama walivyotarajia na pindi wanapowasiliana na wahusika wanakosa
majibu ya uhakika.
“Sisi wengine tangu tuliponunua ving’amuzi
hivi hatujawahi kucheka kwa maana ya kupata huduma za uhakika tunalipa kila
mwezi lakini ukija kuwasha tv ni michenga tu hakuna kiacho onekana, kwahivyo
tumeshachoka kama ZMUX wameshashindwa watuambiaje tutafute ving’amuzi vyengine
mbona vipo vingi tu na viko vizuri lakini tuliona hii ni bidhaa ya nyumbani
wacha tuunge mkono” alisema mmoja miongoni mwa wateja
hao
“Ebwana sisi tuliamini kingamuzi cha ZMUX
kitatusaidia katika masuala ya michezo hususan BACLAYS PREMIER LEAGUE ya pale
Uingerza lakini matokeo yake kwamba King’muzi hichi sisi tunalipia na
tukishamaliza kulipia hapo huoni tela lolote na tuliamua kuchukua king’muzi cha
ZMUX hichi king’muzi ni king’muzi cha Zanzibar
na sisi Wazanzibari tunapenda vitu vyetu lakini matokeo yake imekuwa ni
matapeli na tukiwatafuta wanatuzungusha tu” Haji Khamis Simba mteja ZMUX
Ili kupata ufafanuzi juu ya joto hilo
linalowakabili wateja hao, idawaonline.com ilifanikiwa kuzungumza na mhandishi
kutoka kampuni hiyo ndugu Yusuf Haji Juma, ambapo amekiri kuwepo kwa changamoto
hiyo ya kiufundi katika mnara wa kurushia matangazo wa Kichunjuu Pemba na
kuahidi kufanyiwa matengenezo hivi karibuni.
“Kwanza tunaendelea kuwaomba radhi wateja wetu wote ambao bado wanakabiliana na changamoto ya ukosefu wa huduma zetu kupitia mnara wa KIchunjuu, kwasababu kwa kipindi sasa huduma kupitia mnara wetu wa Kichunjuu zilikuwa zinasitasita kutokana na hitilafu ya ambazo zimejitokeza na tulikuwa tunatoa taarifa kupitia vyombo mbali mbali mpaka kupitia televisheni ya taifa ‘ZBC’ mafundi wetu wa ndani walifanya juhudi kubwa sana kuhakikisha huduma zinarejea tena kwa wakati lakini kwa kuwa haya mambo ya kiufundi yanahitaji utaalamu sana tuka wasiliana na wenzetu kutoka Ujerumani waje watusaidie namna ya kuweza kutatua changamoto hii ambayo imejitokeza katika mnara wetu wa Kichunjuu, hivyo hapa tunapozungumza tumeshapata ujio wa wenzetu kutoka Afrika ya Kusini kwasababu wele wenzetu wa Ujerumani wametuunganisha na ma agenti wao kutoka Afrika Kusini na tayari wamefika nchini kwa kuanza taratibu za kufika Pemba katika mnara wetu wa Kichunjuu kuja kutatua hilo tatizoa ambalo limejitokeza” Mhandisi ZMUX.