AKATWA CHUCHU NA SEHEMU ZA SIRI NA MPENZI WAKE
13 October
0
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linamsaka mwanaume ajulikanaye kwa jina moja la Masudi kwa tuhuma za kumkata chuchu na sehemu za siri na kitu chenye ncha kali mpenzi wake ambaye jina lake limehifadhiwa.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng'anzi, amesema tukio hilo limetokea wilayani Magu katika msitu wa Sayaka ambapo mwanaume huyo anadaiwa kumchukua mpenzi wake huyo na kutekeleza unyama huo kisha kukimbia kusikojulikana.
Tags
Share to other apps