ALIYEMVUTA MUMEWE NYETI ZAKE ANG'ATWA SIKIO

0

 Jeshi la Polisi Mkoani Songwe linamshikilia Nadi Saidi (60) Mkazi wa Kijiji cha Namkukwe Wilayani Songwe kwa tuhuma za kumng'ata masikio hadi kumjeruhi Mke wake Paulina Adam (20) aliyekuwa amemshika na kumvuta Mume wake huyo sehemu za siri baada ya kutokea ugomvi baina yao.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Alex Mkama amesema chanzo cha ugomvi wa Wanandoa hao kinatokana na Mwanaume kumlalamikia Mke wake kuuza mahindi debe moja bila ruhusa yake.

Baada ya malalamiko hayo ndipo ulitokea ugomvi ambapo Mwanamke aliamua kushika sehemu za siri za Mume wake kwa lengo la kujiokoa ambapo Mume nae akiwa katika hatihati za kujinasua ndipo akaamua kumng'ata masikio yote mawili.

Tayari Mtuhumiwa amefikishwa Mahakamani kwa ajili ya kusomewa shtaka lake

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top