ASKARI AKUTWA AMEFARIKI KWENYE KITI AKILINDA MTIHANI WA DARASA LA SABA

0

 

ASKARI wa Jeshi la Akiba (Mgambo), mkazi wa Kijiji cha Manyoni, Kata ya Misozwe wilayani Muheza mkoani Tanga, Yustino Mhina, amekutwa amefariki dunia kwenye kiti wakati akilinda mtihani wa darasa la saba mwaka huu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe, alithibitisha jana kutokea kwa kifo hicho, akibainisha kuwa askari huyo alikutwa na umauti Alhamisi ya wiki hii, siku ya pili ya mtihani huo wakati watahiniwa wa darasa la saba wakifanya mtihani huo wa kuhitimu elimu ya msingi.

Alisema Mhina alikuwa akilinda mtihani huo katika Shule ya Msingi Lumbizi iliyoko Kijiji cha Kwatango, Kata ya Kwemingoji wilayani hapa.

Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kwemingoji, Levina Mushi, alisema askari huyo ambaye tayari mwili wake umeshazikwa, alibainika kupoteza maisha wakati walinzi wenzake walipomkuta asubuhi akiwa kwenye kiti shuleni huko.

Mtendaji huyo alisema mwili wake ulipelekwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza kwa ajili ya uchunguzi na majibu yalionyesha alikunywa dawa zaidi ya kipimo

Alisema mlinzi huyo alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kifafa na alikuwa anatumia dawa kutibu ugonjwa huo

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top