ASKOFU MABOYA AMLILIA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWAOKOE NA NIA OVU YA KUWASAMBARATISHA

0

Mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God amemuomba Rais  wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan awasaidie kuwadhibiti baadhi ya watu wachache walioonesha nia ovu ya kutaka kuondolewa kwa Kanisa hilo lililoko katika eneo la Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Imelda Maboya amesema hayo jana Oktoba 16 katika ibada ya Jumapili iliyofanyika Kanisani hapo, kuwa wako katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 22 sasa ila ameshangazwa na wavamizi waliowavamia kwenye eneo lao la Kanisa zaidi ya mara mbili wakitaka kuwapora ilhali Kanisa lengo lao ni kuiombea jamii ya watanzania.

Maboya amesema kuwa wamejiwekea utaratibu wa kufanya ibada yakuliombea taifa kila baada ya miezi miwili kuliombea taifa lidumu katika amani tuliyonayo ikiwa ni pamojana kuombea viongozi na wananchi kwa ujumla.

Amesema kuwa eneo waliloko ni la Tanzania Steal Pipe (TSP) ambao ndiyo wamiliki halali wa eneo hilo lakini wako hapo kwa ofa maalum iliyotolewa kipindi cha ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma (PCRC) ambako walielezwa kwamba ikitokea panauzwa, watapewa kipaumbele.

"Mahali hapa lilipo Kanisa kulikuwa ni kichaka cha wavuta bangi, walevi na wahuni wengine, uwepo wa Kanisa umesaidia kuiondosha hali hiyo," amesema Maboya.

Ameiomba serikali kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa kuwasaidia ili kuliweka sawa suala hilo.

Sylvia Rweyemamu ambaye ni muumini wa kanisa hilo amesema "mama Samia asikie kilio chetu kwani mbali ya ibada pia tunajipanga kutoa elimu kwa vijana kuhusu sakata la Panya road ambalo ni janga kwa nchi yetu".

Anna Nderumaki amesema ameshangazwa na uvamizi wa watu zaidi ya 100 waliovamia kwenye eneo la Kanisani hilo kwa sababu katika maisha yake hajawahi kuona uvamizi kwenye nyumba ya ibada.

Ezron Matowo amemshukuru Rais Samia Sukuhu kuwa ni msikivu na mwenye huruma, hivyo suala kama hilo ni dogo zaidi kwake kwa sababu anayoyatekeleza yanaonekana.

Muumini Placid Malaki ametumia fursa hiyo kuiomba serikali kuwaongezea eneo hilo kwa ajili ya kufanya ibada kwani wanachotekeleza kwa ajili ya nchi ni kikubwa zaidi.

Mchungaji kiongozi wa kanisa la Calvary Assemblies of God (CAG),Imelda Maboya akizungumza na waandishi wa Habari jana.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top