Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Akson Tulia, amewataka wananchi wa Jimbo hilo la Mbeya Mjini kutokushiriki kumsema vibaya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, pamoja na viongozi wa Jimbo hilo na atakayefanya washughulike nae.
"Kijana yeyote anaungana na mtu yeyote anamsema vibaya Rais ya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia ni Rais wa Nchi lakini pia ni Mwenyekiti wa Chama chetu, asitokee mtu yeyote wa nje ya Chama wa ndani ya Chama halafu wewe ukamtazama shughulika nae, hata Mimi Mbunge wako akitokea mtu kunisema vibaya nyooka nae" alisema Spika Tulia