Mtu mmoja ambaye jina lake bado halijajulikana amefariki baada ya kupokea kipigo kutoka kwa raia alipojaribu kumpora kijana pikipiki,fedha na simu kwa kutumia bastola na sime.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro ACP Simon Maigwa,amesema kijana huyo alipotekwa na jambazi huyo alipiga kelele, ndipo wananchi wakamzingira jambazi huyo na kuanza kumshushia kichapo kabla askari wa doria kufika hapo ambapo walijaribu kumkimbiza hospital lakini alifia njiani.