AUAWA KWA KUPIGWA RISASI BAADA YA KUVAMIA BENKI

0

 

Polisi wamempiga risasi mwanaume aliyekuwa amejihami kwa kisu aliyejaribu kuiba katika Benki ya Equity tawi la Nairobi West mchana peupe.

Katika kisa hicho kilichofanyika Oktoba 11, mwanamume huyo alijaribu kunyakua pesa ambazo zilikuwa zikiwasilishwa benki humo na maafisa wa kampuni ya G4S.

Polisi walisema katika purukushani hizo, mtu anayeshukiwa kuwa jambazi aliwadunga visu watu watatu, maafisa wawili wa usalama na mteja wa benki, ambao walikimbizwa hospitalini. 

Mlinzi mmoja aliripotiwa kuwa katika hali mbaya.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Nairobi James Mugera alisema polisi waliokuwa wakisimamia benki hiyo walijibu kwa kumfyatula risasi jambazi huyo begani na tumboni.

Jambazi huyo pia alikimbizwa katika Hospitali ya Mabagathi, ambapo alikata roho.

Via Tuko News
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top