Kijana mwenye umri wa miaka 22, Nasoro Almas Mkazi wa Mtaa wa Mgulu wa Ndege Manispaa ya Morogoro ameuawa kwa kuchomwa kisu shingoni na Rafiki yake aitwaye Frank (anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-30), chanzo kikiwa ni Nassoro kumdai Tsh.Elfu mbili Frank baada ya kumkopesha siku chache zilizopita.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mgulu wa Ndege, Veronika Michael ametbitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema Mtuhumiwa amekimbia yeye pamoja na Mke wake na anaendelea kutafutwa.
Chanzo Millardayo