Mzee wa umri wa miaka 80 ambaye aliondoka nyumbani miaka 55 iliyopita amewashangaza wanakijiji wa Kathiani, kaunti ya Machakos baada ya kurejea ghafla.
Kulingana na familia ya Kitavi, aliondoka nyumbani mwishoni mwa miaka ya 1960 na hakuna mtu aliyewahi kumwona tangu wakati huo. Jijini Nairobi, alipata kazi ya kuwa bawabu, lakini ikawa ya kuchosha sana kadri miaka ilivyozidi kumuandama.
Aliacha kazi hiyo na kuanza kuombaomba katika mtaa wa Majengo. Msamaria wema kwa jina Christine Ndanu, mtangazaji wa Musyi FM, alitangulia kumuunganisha mzee huyo na familia yake. Kitavi alikaribishwa kishujaa aliporudi nyumbani.
Picha za Musyi FM kwenye Facebook zilimuonyesha akiendeshwa kwenye gari la kisasa ambalo pia lilitanguliwa na pikipiki. Walipofika, jamaa wa marafiki walimzunguka, wote walifanya maombi na sherehe zilianza kwa kasi.
Kwingineko, Wilson Numbi ambaye tayari alikuwa ameoa wake wawili na kuzaa watoto 10 akiwa na umri wa miaka 34 lakini badala ya kuwa nguzo katika familia aliuza kila kitu akaondoka huku akiwaacha bila chochote. Baada ya miaka 49, picha za mzee huyo zilizosambaa mtandaoni zilifahamisha familia yake yenye wasiwasi kuhusu aliko baba yao.
Tangu wakati huo amekaribishwa nyumbani kwa msamaha bila kujali makosa yale aliyofanya hapo awali.
Chanzo: Tuko