Mkuu wa wilaya ya shinyanga Jasinta Mboneko amepiga marufuku uwepo wanawake wanaofanya biashara ya Ngono maarufu kama 'Madada Poa' kwenye baadhi ya vijiji na maeneo wilayani humo kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo kwenye maeneo ya vijijini.
Amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji na kata ya Nyida wilaya ya shinyanga vijijini, amesema uwepo wa wanawake wanaojiuza kwenye baadhi ya vijiji kumekuwa na mmomonyoko wa maadili na wizi wa mazao kwa wakulima wa vijiji hivyo, kutokana na wadada hao kuwalaghai wakulima, kuwaibia mazao na kupelekea ndoa nyingi kuvunjika.