Wananchi wanaokwenda katika vituo vya afya wameombwa kuwa na subra katika kusajili taarira zao kupitia mfumo mpya wa kuhifadhia huduma za afya mtandaoni ili kufanikisha lengo la uanzishwaji wa mfumo huo.
Ombi
hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali Mtandao Ndg. Said
Seif Said, katika ziara ya kutembelea katika hospitali tatu za Chake Chake,
Abdalla Mzee Mkoani na Vitongoji katika kukagua namna mfumo huo unavyofanyakazi
sambamba na kusikiliza changamoto mbali mbali zinazotokana na mfumo huo wa
huduma za afya mtandaoni.
Amesema
mfumo wa huduma za afya mtandaoni ni mfumo imara ambao utaweza kuhifadhi
taarifa za mgonjwa kwa usahihi zaidi pamoja kuepusha wimbi la mrundikano wa
wagonjwa pindi wanapohitaji huduma.
“Tunakiri kwamba huu ni mfumo mpya lakini mfumo bora na imara sana kuliko mifumo mengine yote, kwasababu mfumo huu una uwezo wa kuhifadhi taarifa za uhakika na kwa wakati za lakini pia ni mfumo ambao utaweza kuepusha opotevu wa dawa, mrundiko wa wagonjwa, wafanyakazi, kupunguza wingi wa mifumo kwenye hospitali na vituo vya afya” Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali Mtandao Said Ali Sa
Kwa upande, kaimu Mganga Mkuu wa hospital ya Mkoani Daktari Said Ismail Ali, Said, amesema licha ya mfumo huo kuwa mfumo bora zaidi katika kuhifadhi taarifa za wagonjwa lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa vitendea kazi, watoa huduma jambo ambalo linapelekea mrukano wa wagonjwa.
Harun Maisara Mahkum ni mkuu wa usajili hospitali ya rufaa ya Abdalla Mzee Mkoani, amesema watoaji wa huduma katika mfumo huo bado wanakabilkiwa na changamoto ya uhaba wa vifaa pamoja na kutokuwa na uzoefu wa kutosha wa matumizi ya komputa katika kuhifadhi taarifa.
“Kwakweli mfumo huu ni nzuri sana kwani mgonjwa akishasajiliwa kwa mfano hapa hospitali ya Abdalla Mzee akienda hospitali nyengine yoyote anaonesha kadi yake na taarifa zake zote zinaonekana lakini changamoto kubwa inayotukabili ni uhaba wa vitendea kazi pamoja na kutokuwa na uzoefu wa kutosha wa utumiaji wa komputa katika kuhifadhi taarifa za mgonjwa” alisema
Harun Maisara Mahkum ni mkuu wa usajili hospitali ya rufaa ya Abdalla Mzee Mkoani.
Nae, Mkuu wa MKoa wa Kusini Pemba Mheshimiwa Matar Zahor Massoud, amewaahidi watendaji hao wa Wakala wa Serikali Mtandao kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na huduma za afya mtandaoni ili waweze kufahamu kuhusu huduma hiyo.
“Kwakweli
dhamira na miono hii ya mheshimiwa Rais ni njema na tunapaswa kuunga mkono
juhudi hizi za msheshimiwa Rais katika kuwaletea wananchi maendeleo, kwahivyo na
sisi watendaji wa Serikali kuanzia ngazi ya Mkoa na Wilaya ni wajibu wetu sasa
kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mfumo huu kwasababu ni rahisi kwafikia na wao
huwa wanakuja katika ofisi zetu pale wanapohisi kuna mambo yanawakwaza, hivyo
basi ni waahidi kuifikisha elimu ya huduma za afya mtandaoni kwa wananchi wote”
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba
Ali
Hamad Omar, ni mwananchi mkaazi wa Wete akiwa akiwa katika hospitali ya Abdalla
Mzee Mkoani, amesema wamefurahishwa na uanzishwaji wa mfumo huo mpya wa huduma
za afya mtandaoni kwani utawarahisishia upatikanaji wa huduma za afya kwa
urahisi pamoja kuepuakana na changamoto ya kukaa foleni kusubiri kusajiliwa kwa
njia ya madaftari kama ilivyokuwa hapo awali.
“Binafsi nimeridhishwa sana na huu mfumo wa kuhifadhi taarifa za wagonjwa kwa njia ya mtandao kwasababu utaturahisishia kupata huduma kwa urahisi baada ya kusajiliwa kwasababu kitendo cha kuonesha tu kadi yako hospitali yoyote unayokwenda kinyume na ile hospitali uliyosajiliwa kisha taarifa zako zote zinaonekana ni jambo la kufurahisha mno, niwaombe tu wananchi wenzangu kuwa subra na uvumilivu pindi wanapokuja hospitali na kutaka kusajiliwa kwenye mfumo huu” Alisema mwananchi huyo
Massoud Ali Nassor, ni mkuu wa kituo cha hospitali ya Vitongoji, ameishukuru taasisi ya Wakala Serikali Mtandao kwa kuanzisha mfumo huo mpya wa kuhifadhi taarifa za wagojwa kuptia mtanda, ambapo amesema mfumo huo unasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuhifadhi taarifa za wagonjwa na dawa.
Sambamba
nashukurani hizo, amesema mfumo huo unakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo changamoto
ya huduma ya mtandao (Internet) kupoteza taarifa za mgonjwa wakati umeme
unapozimika, hivyo basi ameuomba uongozi wa taasisi hiyo kuzifanyia kazi
changamoto hizo ili kuboresha huduma hiyo.
“Awali wakati tukiwa katika ule utaratibu wa kuhifadhi taarifa za wagonjuwa kwenye madaftari tulikuwa tunakabiliwa na tatizo kubwa la upotevu wa dawa lakini sasa tunaona kupitia mfumo huu kila kitu kimerekodiwa na kuhifadhiwa hata kidonge kimoja cha dawa hakiwezi kupotea, kwahivyo tunaona na jinsi huu mfumo umekuja kusaidia sana kuhifadhi taarifa kwa umakini na usahihi mkubwa sana licha kwamba bado tunakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kupotea kwa taarifa pindi umeme unapozimika kwasababu hizi komputa hazina uwezo wa kuhifadhi umeme hata dakika tano kwahivyo tunaomba kufanyiwa mpango tukapata kifaa ambacho kitaweza kuhifadhi umeme kwenye huu mfumo pindi umeme unapozimika, changamoto nyengine ni suala la internet baadhi ya wakati internet inakuwa low sana kwahivyo watoa huduma wanashindwa kutoa huduma kwa haraka hadi pale internet itakaporudi” Massoud Ali Nassor, mkuu wa hospitali ya Vitongoji
Akiahidi
kuzifanyia kazi changamoto zinazoukabili mfumo huo, mkuu wa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Ndg. Mohammed Habib Ally,
amesema Wizara hiyo imejipanga kuhakikisha kuzitatua changamoto zote
zinazoukabili mfumo ikiwemo kuongeza vitendea kazi, watoa huduma pamoja kutoa
elimu kwa wananchi ili kuhakikisha lengo la uanzishwaji wa mfumo huo linafikiwa.
Huduma
ya afya mtandanoni imeanzishwa rasmi mwezi Agosti, 2022 ikiwa ni sehemu ya
malengo ya utekelezaji wa mkakati wa digitali wa miaka mitano ambao ulianza
mwaka 2020, kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya kwa jamii kwa
kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA.
Mkakati
huo wa digitali za afya una maeneo 25 ya utekelezaji ambapo mfumo wa unaotumika
kutolea huduma za kwenye hospitali na vituo vya afya ni moja ya vipaumbele.
Mfumo wa EMR uliandaliwa na kutolewa mafunzo kwa watumiaji, kwa hatua ya mwanzo kuanzia mwezi wa September 2022, mfumo huo ulianza kutumika kwenye hospitali tano (5) za Pemba ambazo ni Chake Chake, Micheweni, Wete, Vitongoji na Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani.