HATIMAYE BINTI AKUBALI KUOLEWA NA JAMAA ALIYEMSOMESHA CHUO KIKUU

0

 

Peter na Agatha hivi majuzi walifanya harusi kubwa katika Kanisa Kuu la Kristo Bugembe nchini Uganda, kilele cha uhusiano ulioanzia chuo kikuu 


Jambo ambalo wengi hawajui ni kwamba bwana harusi alihangaika kwa miezi kadhaa kumshawishi bi harusi mtarajiwa akubali kuchumbiwa 


Kwa hakika, ilimbidi athibitishe kwamba alikuwa makini kutaka kujenga uhusiano wao kwa kumtambulisha kwa familia yake bali pia kulipa ada ya hosteli yake kwa mwaka mmoja 


Peter alikuwa karibu kumaliza masomo yake ya chuo kikuu alipoanza kupanga mipango ya mustakabali wazi wa maisha mbele yao.

Mbali na kupata kazi, kuimarika kifedha na, kwa matumaini kupata mali, alijua kabisa kwamba alitaka mke ashiriki katika harakati zake.


Kana kwamba majaliwa yamesikia sala yake ya kimyakimya, Peter alikutana na mara moja akavutiwa na msichana mrembo wa Uganda anayeitwa Agatha. Aliiambia mywedding.co.ug kwamba alijua kwamba alikuwa amempata mwanamke wa ndoto zake mara tu alipoweka macho yake kwa mwanafunzi huyo wa mwaka wa pili.


Tatizo pekee lilikuwa kwamba Agatha alilelewa kutoka katika nyumba ya Kiungu na, baada ya kuumizwa moyo hapo awali, ilikuwa vigumu kwake kukubali kujiingiza katika uhusiano mwingine. "Nilifanya ziara nyingi katika Hosteli ya Baskon ambako Agatha aliishi, nilitumia muda wangu kukaa naye, tulijivinjari katika migahawa ya mjini na iliyoko nje jiji," alikumbuka.


Ili kudhibitisha kuwa alikuwa na nia ya kuanza uhusiano wa mapenzi na Agatha, Peter anafichua kwamba alimtambulisha kwa familia yake. Kulingana naye, wazo la kumtambulisha nyumbani ilikuwa ni kuhakikisha 'anamnasa' dada huyo ndiposa asinyakuliwe na mwingine. Kando na hayo, jamaa alianza kumlipia mrembo wake ada ya hosteli kwa mwaka mmoja alipokuwa akiishi akiwa chuoni.


 Kadiri siku zilivyosonga, wanandoa hao walianza kusali pamoja na wangeshiriki safari za kiroho kama vile kufunga pamoja. Sherehe ya kutambulishwa kwao ilifanyika Desemba 2021 na kufuatiwa na harusi ya kufana iliyoandaliwa mnamo Septemba 4, 2022.


Wanandoa hao wapya sasa wanatazamia kufurahia maisha yao katika ndoa hadi watakapotenganishwa na kifo.


Chanzo: Tuko Swahili

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top