HILI NDIO AGIZO LA WAZIRI GWAJIMA KWA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII....

0

 Waziri wa maendeleo ya jamii,jinsia wanawake na makundi maalum Dkt. Dorothy Gwajima amewataka maafisa maendeleo ya Jamii kutoa Elimu kwa wanawake waishio vijijini ili kupata mikopo ambayo inatolewa na Serikali.

Waziri Gwajima ameyasema hayo Mjini Morogoro wakati wa maadhimisho ya Kimataifa ya Mwanamke anayeishi kijijini ambayo yamefanyika katika Kijiji cha Mang’ula B Wilayani Kilombero Mkoani humo.

Amesema bado wanawake wengi wa vijijini hawana elimu ya mikopo pamoja na kufahamu majukwaa ua kiuchumi hivyo maafisa maendeleo ya jamii wanatakiwa kutoa elimu kwa kundi hilo ili lijikomboe kiuchumi.Aidha Waziri Gwajima ametoa wito kwa wanawake kutofumbia macho vitendo vya kikatili ambayo wanafanyiwa nyumbani kwani vitendo hivyo vimekua vikiwaathiri kimwili na kiakili.

Kwa upande wake Amina Juma mkazi wa kilombero anayejishughulisha na kazi ya mama lishe anasema suala la kukaa bila Kazi ni moja ya sababu ya kuongezeka matukio ya ukatili wa kijinsia kwa Wanawake.

Anasema anamshukuru Mume wake kwa kumruhusu kufanya Kazi za ujasiriamli kwani inasaidia kuongeza uchumi wa familia ambapo anasema kuishi Kijijini sio lazima utegemee kilimo peke yake.

Naye mwenyekiti wa shujaa wa maedeleo na ustawi jamii Tanzania ( SMAUJATA) Mkoa wa Morogoro Bwana Milavan Charles amesema kwa Sasa wameanza mkakati wa kupita shule zote za mkoa Morogoro ili kutoa elimu ya ukatili kwa watoto.

Amesema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni wazazi wamekua kikwazo kwa kushindwa kutoa ushahidi mahakamani Jambo ambalo linarudisha nyuma jitihada za Serikali katika kupambana na ukatili wa kijinsia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top