HIVI NDIVYO WANAFUNZI WALIVYOZUIA UDANYANYIFU WA MTIHANI ISIKUPITE HII

0

 

Picha za wanafunzi wa  Chuo Kikuu cha Legazpi, nchini Ufilipino wakiwa wamevalia kofia za kuzuia udanganyifu walipokuwa wakifanya mitihani yao ya mwisho zimesambaa mitanadoni kote ulimwenguni.

Wanafunzi wote walifika kwenye jumba la mtihani wakiwa na kofia aina tofauti ambazo walitengeneza nyumbani kwao kwa kadibodi, masanduku ya mayai na vitu vingine. Hii ni kufuatia agizo la usimamizi wa shule.

Wanafunzi wengine walivalia miwani mirefu ili kuwazuia  kutazama vijitabu vya majibu vya majirani wao au kuwauliza maswali wakati wa mtihani.

Picha hizi  ziliwafanya walioziona kutoficha vicheko vyao kwenye mitandao za kijamii huku wengi wakionyesha kupuuza hatua hiyo na wengine kuunga mkono ubunifu uliotumika.

Mwalimu anayefahamika kama Mary Joy Mandane-Ortiz aliyebuni njia hii, akizungumza na kituo cha habari cha BBC, alisema kwamba amekuwa akitafuta njia mwafaka na itakayohakikisha kuna uadilifu na uaminifu katika darasa lake.

Profesa huyo alisema wazo hilo, ingawaje baadhi walipuuza  lilikuwa lenye ufanisi mkubwa wa kupindukia.

Picha za  wanafunzi hao wakiwa wamevalia kofia walizotengeneza kutumia ubunifu wa hali ya juu ziliwapendeza wengi.

Pia inasemekana walimu wakuu wa shule na vyuo vikuu katika maeneo mengine ya nchi hiyo wanalenga kuiga mbinu hiyo kuzuia udanganyifu wa mitihani shuleni.

Prof Mandane Ortiz alisema wanafunzi wake walifanya vyema zaidi mwaka huu, baada ya kuanzisha mbinu hiyo na kuwekwa kwa masharti magumu ya mitihani kwani iliwafanya wanafunzi kusoma kwa bidii zaidi.

Wengi wao walimaliza majaribio yao mapema, aliongeza - na hakuna mtu aliyekamatwa akidanganya mwaka huu. 

Chanzo - BBC

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top