Watu wawili waliotambulika kwa majina ya Ibrahim Shabani mwenye umri wa miaka 21, na Mussa Bakari mwenye umri wa miaka 28, wamefariki dunia Wilayani Masasi Mkoani Mtwara, baada ya kupigana kwa kutumia magogo wakati wakigombea mwanamke anaefahamika kwa jina la Khadija Msamati.
Wakizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi ACP Nicademus Katembo, amesema tukio hilo limetokea juzi September 29, 2022 majira ya saa sita usiku katika kijiji cha Mkangaula kata ya Namalenga Wilayani Masasi.
ACP Katembo amesema tukio hilo limesababishwa na wivu wa mapenzi na baada ya kufanyika kwa uchunguzi wamebaini marehemu hao walikuwa kwenye ugomvi wa kugombea mpenzi wao ambaye baada ya tukio hilo alitoweka na kwenda pasipojuilikana.
Miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi na daktari na kubainika kuwa chanzo cha kifo hivyo ni kuvuja damu kwa wingi mwilini.
Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara limesema linaendelea na juhudi za kumsaka mwanamke huyo kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Chanzo. Wasafitv