SERIKALI YATOA TAMKO WALIOTAPELIWA KALYNDA E COMMERCEE

0

Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa kutokana na malalamiko ya baadhi ya wananchi kulalamika kutapeliwa fedha zao na kampuni waliyoeleza ni Kalynda E Commerce kwa njia ya mtandao, Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kwa kushiriana na taasisi nyingine za kiuchunguzi na za kifedha wameanza kuchunguza malalamiko hayo ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Akizungumza wa Waandishi wa Habari Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime amesema Wakati hatua hizo zinaendelea kuchukuliwa Jeshi la Polisi linatoa tahadhari tena kwa mara nyingine kwa Watanzania kuwa makini na utapeli wa aina hiyo huku akiwataka Mwananchi wanaotaka kuwekeza kwenda kwenye taasisi za kifedha kama mabenki zilizoanzishwa kisheria na ofisi za wanaoendesha zinajulikana. Pia Vyama vya Ushirika ambavyo vinaanzishwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya ushirika

"Kila mmoja atambue, kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani kote wahalifu wanatumia maendeleo hayo kupitia mitandaoni kutapeli mamilioni ya fedha kwa maneno ya kuvutia kuwa utapata fedha nyingi katika kipindi kifupi kama utawekeza kiasi fulani cha fedha. Wengine wanajifanya kuuza bidhaa za aina mbalimbali au magari.

"Jambo la kujiuliza, kama hayo wanayokuvutia nayo ni ya kweli, kwanini wasiwahamasishe ndugu zao na ukoo wao wakatajirika kama wanavyo kudanganya?"

"Hivo huruma kwako wewe ambaye hamfahamiani inatoka wapi? Ni lazima kila mmoja wetu atambue, kuna matapeli na usalama wa fedha au mali yako unaanza kwanza na wewe mwenvewe. Ni vizuri kutambua hakuna utajiri au kujipatia fedha kwa njia rahisi kiasi hicho bila kutoka jasho kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi."

"Hata kama umevutiwa kiasi gani na uwekezaji fedha kama wanavyo tangaza mitandaoni, fanya utafiti kwanza, kwa kuuliza mamlaka zinazosimamia kupata ukweli. Tumia viongozi wa serikali au Jeshi la Polisi kuuliza badala ya kuongozwa na tamaa.

Aidha, SACP David Misime amewataka mwananchi pale watakapo baini kampuni zenye mwenendo wa aina hiyo wasisite kutoa taarifa mapema ili hatua stahiki zichukuliwe.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top