KAMANDA WA POLISI ASEMA MAREHEMU ALIKUWA AKIOMBA PENZI KWA MKE WA MASANJA

0

 


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne amesema uchunguzi wa awali wa Polisi kuhusu tukio la Katibu wa Mke wa Masanja Mkandamizaji kujiua kwa kujinyonga umeonesha kwamba Marehemu na Mke wa Masanja hawakuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi.


Akiongea na LEO TENA ya Clouds FM, Kamanda Muliro amesema — "Ni kweli uchunguzi wa awali unaonesha mawasiliano yanaonesha huyo Marehemu akiwa anaomba, akiwa anataka, anaomba mahusiano ya kimapenzi na huyu Mtu ambaye inadaiwa ni Mke wa Masanja, ni kweli pia kabla ya tukio Mke wa Masanja akiwa na Mama mwingine walikwenda nyumbani kwa Marehemu kumueleza kwamba yule Mke hataki msg za namna ile na hataki mahusiano na yeye"

"Ni kweli pia yule Mtu alifadhaika baada ya kuelezwa waziwazi kwamba yule ni Mke wa Mtu na hataki mahusiano nae, sasa mtitiriko wa visa hivyo unatoa nafasi ya kutokuwa na shaka na mazingira ya kifo kile, bila shaka atakua amejinyonga kwa sababu mbalimbali za fikra zake au sababu nyingine yoyote lakini hata hivyo bado Jeshi la Polisi haliwezi likaishia kwenye ushahidi wa awali ambao umeonekana.... mwisho huwa ni kufanya uchunguzi wa kitaalamu" ——— 
amesema Kamanda Muliro. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top