KASISI AONYA NGUO FUPI ASEMA ZINAWAFANYA WANAUME WASHINDWE KUSALI

0

 

Kasisi wa Kikatoliki wa parokia ya St Peter’s Oyugis Homa Bay, Padre Tom Nicholas Mboya ameelezea wasiwasi wake kuhusu mavazi wanayovalia baadhi ya waumini wa kanisa hilo, ambao anasema ni utovu wa maadili.


Padre Mboya alisema kamwe hawezi kunyamaza wakati kondoo wake wanapopotea, ripoti ya The Standard ilisema. Hili lilidhihirika Jumapili iliyopita wakati wa ibada ya maombi katika kanisa lake. 


Padre Mboya, ambaye aliongoza ibada aliwaambia wanawake na wasichana wanaoenda kanisani wakiwa wamevalia mavazi yasiyo ya heshima waache tabia hiyo mbovu.


“Kuna baadhi ya wanawake ambao huja kanisani wakiwa wamevalia mavazi ambayo si tofauti na wale wanaotembea katika mitaa ya mji wa Oyugis. Ukweli wa mambo ni kwamba hawana adabu,” alisema. Alisema kuwa uvaaji usio na staha huwavuruga watu wakati wa maombi kanisani. Wanawake kama hao wamevaa kwa njia ya kuwatia majaribuni wanaume. "Kukosa kufunika sehemu fulani za mwili na kuja kanisani ni kuwatatiza wengine akili," Kasissi Mboya alisema. 


Mtumsihi huyo alikumbuka siku moja alipomwona msichana akiwa amebeba Biblia ambayo ilikuwa inaenda kusomwa wakati wa ibada ya maombi akiwa amevalia mavazi ambayo "yalizua maswali mengi". Msichana alivaa T-shati iliyoandikwa: "Ikiwa unanipenda, tabasamu pamoja nami." “Kilichoandikwa kwenye fulana hiyo hakikuwa ch kupendeza kwa sababu watu wazima wangeweza kutafsiri kuwa kinamaanisha kinyume na mapenzi ya Mungu. Hata hivyo, ujumbe huo unaweza kuonekana kuwafurahisha watoto,” kasisi huyo alisema.


Aliwataka wazazi kuwa makini katika kuhakikisha watoto wao wanavaa kwa heshima. Kasisi huyo aliwataka waumini kuzingatia kanuni za mavazi za Kanisa Katoliki kwa ajili ya Chama cha Wanaume Wakatoliki, Jumuiya ya Wanawake Wakatoliki na kwaya. "Ninachotaka ni watu wavalie mavazi ya heshima. Hii haimaanishi unanunua nguo za gharama kubwa. Vaa tu nguo zenye heshima zinazofunika mwili wako vizuri,” alisema. 

Chanzo: TUKO.co.ke 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top