Mwisho wa wiki iliyopita kulikuwepo na uvumi wa sakata la kujitoa uhai kwa katibu wa kanisa la Fell Free Church la aliyekuwa Mchekeshaji na Mchungaji Masanja Mkandamizaji kutoka Nchini Tanzania.
Taarifa zilisema kuwa katibu huyo
alijitoa uhai kutokana na kujuilikana kwa kashfa ya kutoka kimapenzi na mama wa
kanisa ambaye ni mke wa wa Mchungaji Masanja Mkandamizaji.
Ujumbe mrefu uliovujishwa kutoka kwa
marehemu kabla ya kifo chake unaeleza kwa mapana sababu za kujitoa uhai katika
sakata ambalo sasa limejumuisha mambo mengi ikiwemo suala la kuchepuka na mama
wa kanisa.
Barua hiyo ilionekana kumuandikia
mwanamke mmoja ambaye bado haijabainika kama ni kweli ni mke wake Mchungaji
Masanja.
“Asante kwa kunipenda kipindi chote
hakika umenipa upendo ambao umeacha alama moyoni mwangu ambao kila nikijaribu
kuifuta nimeshindwa sioni upendo wako wa mwanzo hivyo nimebaki kuumia moyoni” Sehemu ya barua
Mchungaji Masanja ambaye kila
Jumapili huwa anahubiri katika kituo cha Wasafi fm Radio, hakuhudhuria katika
kipindi hicho kutokana na suala hilo tata ambalo linazidi kuchemka haswa kwenye
mitandao ya kijamii.
Kupitia ukurasa wa Instagram,
Mchungaji Masanja alipakia video yenye picha ya pamoja na mke wake wakionekana
katika mkao wa kuomba na kusujudu na kuachia ujumbe wenye utata ambao wengi
waliuwambatanisha na sakata hilo la kujitoa uhai kwa katibu katika kanisa lake.
Baada ya watu zaidi ya laki mbili
kufurika katika ukurasa wa huo Mchungaji Masanja, na kuachia maoni mbali mbali,
Mchungaji Masanja Mkandamizaji aliifuta maudhui hayo lakini kuna baadhi ya wale
waliobahatika kuinakili na ilikuwa na maneno yafuatayo
“Kila kazi ina gharama yake. Acha
tulipe gharama ya tulichoitiwa. Nakupenda mpaka pumzi yangu ya mwisho mke wangu.
Hili nalo litapita. Tuombeeni nasi tunaomba. Mtetezi wangu yu hai” Aliandika Mchungaji Masanja
Katika maneno haya, wengi walionekana
kukisia kuwa Mchungaji huyo alikuwa anatia roho ya kiume kusimama na mke wake
wakati wa kipindi hichi kigumu ambacho kimezua hisia tofauti za kumsaliti mume
wake na mfanyakazi wa kanisa hilo.
Wengine walisema kuwa huenda katibu
huyo alijiua sit u kutokana na mzozo wa kimapenzi bali pia kutokana na msongo
wa akili.
Inashauriwa kuwa kama umepetwa na
hali inayopelekea kupatwa na tatizo la msongo wa mawazo kwa kukwazwa na mambo
mbali mbali washirikishe ndugu, marafiki, washauri nasaha, madaktari pamoja
wanasaikolojia ili kupata ufafanuzi juu ya kile kinachokukwaza.
Kwa msaada wa ushauri nasaha piga
nambari hizi bila ya maliupo 1199.