Katika muendelezo wa kusikiliza mashahidi kwa upande wa walalamikaji dhidi ya kesi ya tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la tano mwenye umri wa miaka 11 inayomkabili mwalimu wa skulia ya msingi Madungu, shahidi wa nne ambaye ni shahidi wa mwisho, upande huo umekamilisha ushahidi wake baada ya askari mpelelezi kutoa ushahidi mbele ya mahakama hiyo.
Akitoa ushahidi mbele katika kiriri cha mahakama hiyo, shahidi huyo amesema kwa mujibu upelelezi uliofanywa na jeshi la Polisi umegundua kuwa daftari la mahudhurio la Skuli
lilionesha kuwa siku ambayo mwalimu huyo anatuhumiwa kufanya kitendo cha
kumbaka mwanafunzi huyo aliingia kazini.
“Mheshimiwa hakimu kwa mujibu wa upepelezi ambayo
jeshi la Polisi uliufanya ni pamoja na kufika skuli ambayo anasomesha
mshitakiwa na kupatiwa daftari la mahudhurio ambapo limeonesha kuwa siku ya
tukio mshitakiwa iliingia kazini” Alisema
Aidha,
mpelelezi huyo alisema kuwa upelelezi uliofanywa na jeshi la Polisi umebaini
kuwa kutokana na mazingira darasa ambalo muathirika alidai kuwa mshitakiwa
aliitumia darasa hilo kumfanyia vitendo vya ubakaji, mshitakiwa anaweza
kulitumia darasa hilo kufanyia vitendo hivyo kutokana na mazingira ya faragha
ya darasa hilo na skulini hapo.
“Upelelezi
uliofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kuwa kutokana na mazingira ya darasa
ambalo muathirika alidai kuwa alikuwa mwalimu analitumia kumbaka, jeshi la
Polisi limejiridhisha kuwa mazingira ya faragha ya darasa hilo pamoja na mazingira
ya skuli yenyewe mshitakiwa anaweza kulitumia darasa hilo kufanya vitendo hivyo”
Askari mpelelezi.
Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na askari
mpelelezi mahakamani hapo hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma, amesema
ameridhishwa na ushahidi huo na kumuamuru mshitakiwa kurudi rumande hadi tarehe
12.10.2022 kwa ajili ya kutoa uamizi mdogo.
“Kutokana na ushahidi ambao ametolewa na shahidi mahakama
imeridhishwa na ushahidi huo na mshitakiwa atarudi tena rumande hadi tarehe
12.10.2022 kwa ajili ya uamuzi mdogo wa shitaka hili” Alisema
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa siku ya tarehe 12.08.2022 majira ya 11:30 za jioni huko katika Skuli ya Msingi Madungu, Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, mshitakiwa alimbaka mwanafunzi wa darasa la tano mwenye umri wa miaka 11, jambo ambalo ni kosa kisheria kwa mujibu wa kufungu cha sheria ya adhabu nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Ikumbukwe kuwa kesi hiyo ilianza kutajwa mahakamani hapo Agosti 05.2022.