KIJANA AJERUHIWA VIBAYA NA SHOTI YA UMEME WAKATI AKIKATA NGUZO YA UMEME KWA SHOKA- TABORA

0

Kijana mwenye umri wa miaka 24 aliyefahamika kwa jina la Kigodi Juma mkazi wa kijiji cha Nkiniziwa kilichopo Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora amejuruhiwa vibaya katika maeneo ya mwili wake baada ya kuburuza na shoti ya umeme wakati alipokuwa akifanya hujuma ya kukata nguzo ya umeme kwa kutumia shoka .


Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo Afisa mtendaji wa kata ya Nkiniziwa Hamisi Bundu amesema kijana huyo alitenda tukio hilo usiku wa kuamkia Oktoba 10,2022 ambapo kunako majira hayo ya usiku walishitushwa na kukatika kwa huduma ya umeme.

Amesema kijana huyo kabla ya kuanza kukata nguzo hiyo alirusha waya uliokuwa umefungwa vipande vya miti kwa ajili ya kupigisha shoti ili umeme uweze kukatika ili apate urahisi wa kuangusha nguzo hiyo bila wasiwasi wa kujeruhiwa na umeme pasipo kujua kama umeme bado ulikuwa haujakatika .

Kijana huyo ambaye alishambuliwa vibaya na shoti ya umeme alikimbizwa katika kituo cha afya Busondo ambacho kipo jirani na kijiji hicho ambapo kwa sasa anaendelea na matibabu huku kaimu Mganga wa kituo hicho cha afya Juma Sosoma akieleza licha ahuweni aliyonayo kwa sasa ataandikiwa rufaa ya kwenda katika hospitali kubwa kwa ajili ya vipimo zaidi vya ndani ya mwili kutokana na kuumia vibaya katika maeneo ya miguu,shingo ,usoni na kwenye mikono.

Wanachi wa kijiji hicho cha Nkiniziwa wamesema mpaka sasa bado wanaendelea kuathirika na ukosefu wa huduma ya umeme huku tukio hilo la kukatwa kwa nguzo likitajwa kuwa ni la pili katika eneo hilo hilo.

Kaimu meneja wa shirika la umeme nchini TANESCO katika Mkoa wa Tabora Mhandisi Hamisi Maganga amesema shirika linaendelea na ufatiliaji wa kina dhidi tukio hilo huku akiwaonya vikali wananchi dhidi vitendo vya kuhujumu miundo mbinu ya umeme .
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top