KILA MTOTO ATENGEWA Tsh.1000 KUKABILIANA NA LISHE H/MJI MKAMBAKO,,,WATENDAJI WASAINI MKATABA

0

 Na Bilgither Nyoni-Makambako

Katika kukabiliana na Lishe duni, Halmashauri ya Mji wa Makambako Imetia saini Mikataba ya lishe itakayotumika kwa miaka nane baina ya ofisi ya Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Kata 12 zilizopo katika Mji wa Makambako.

 

Baadhi ya maafisa watendaji wakielekezwa jinsi ya kusaini Mkataba wa Lishe.

Kabla ya Utiaji saini wa Mikataba hiyo,Mada zinazohusu lishe ziliwasilishwa na Katibu wa Afya wa Halmashauri ya Mji Makambako,Benedict Musiba sambamba na Afisa Lishe Meckfrida Mmari ili kuwajengea uelewa Watendaji juu ya majukumu yao katika usimamizi wa Lishe kwenye Kata zao ili kufanikisha uboreshaji wa lishe kwa watoto chini ya miaka mitano.

 

Mkoa wa Njombe unakabiliwa na tatizo la Udumavu kwa asilimia 53.6, hali inayoelezwa kuchangiwa na lishe duni kwa watoto chini ya miaka mitano ambapo Halmashauri ya Mji Makambako asilimia 0.9 ya watoto wana tatizo la udumavu na asilimia 0.7 wanakabiliwa na tatizo la ukondefu, unaosababishwa na ukosefu wa virutubisho muhimu katika chakula.

 

Ili kukabiliana na tatizo la udumavu na ukondefu kwa watoto chini ya miaka mitano,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako,Kenneth Haule ametoa agizo kwa Afisa lishe na Maafisa elimu Msingi na Sekondari kuhakikisha kila shule inakuwa na vitalu vya mbogamboga na matunda badala ya maua,ili zitumike katika vyakula vya wanafunzi shuleni.

 


amemuagiza Kaimu  Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Makambako,Dkt. Ally Senga kuhakikisha Watendaji wa Kata,Mitaa na Vijiji wanashirikiana na Kamati za Afya katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali yanayohusu afya na lishe katika Mitaa na vijiji ili kuwajengea uwezo Watendaji wa kutoa elimu ya lishe kwa wananchi.

Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa makambako Ally Senga Amesema kuwa wataalamu wa Afya watashirikiana pia Na sekta ya kilimo na mifugo kwa kuwa zinaingiliana katika kutoa elimu sahihi ya lishe kwa jamii ili waweze kupata lishe iliyobora.

Nao baadhi ya watendaji wa kata akiwemo Daria kilasi wa kata ya kitisi pamoja na Boniface mtawa wa kata ya mahongole wameahidi kuweka agenda ya kudumu katika kutoa elimu kuanzia ngazi ya chini.

Pamoja na hayo Halmashauri ya Mji Makambako imetenga kiasi cha zaidi ya Mil. 26 kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 ,ambapo mapato ya ndani ni Mil. 18 ikiwa ni fedha kwa ajili ya lishe ya   watoto  shuleni, ambapo kila mtoto anatengewa wastani wa shilingi 1,000 ikiwa ni agizo la Serikali.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top