KINYOZI AKUTWA AKIFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI CHUMBANI..ATIWA MBARONI

0

 Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Ilenza Halamashauri ya Buchosa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza (jina linahifadhiwa) aliyekutwa chumbani akifanya mapenzi na fundi kinyozi amedai alifanya hivyo kutokana na ushawishi wa kinyozi huyo.

Picha kutoka maktaba

Akisimulia tukio hilo baada ya kufumwa akitokea chumbani kwa kinyozi huyo Alhamisi, Oktoba 13, 2022, mwanafunzi huyo alisema alikumbana na ushawishi wa kinyozi huyo alipofika eneo lake la kazi kwa ajili ya kupunguza nywele kabla ya kwenda shuleni akitoka likizo nyumbani kwao wilayani Magu.

“Sikutaka kwenda shuleni nikiwa na nywele ndefu ndio maana niliamua kupitia kwa kinyozi ninyoe; baada ya kunyoa, yule kinyozi alinishawishi nisiende shule siku hiyo kwa ahadi ya kunisaidia fedha za matumizi,” alisema mwanafunzi huyo.


Alisema kutokana na ushawishi, aliambatana na kinyozi huyo hadi chumbani kwake walikolala hadi siku iliyofuata huku akilazimishwa kufanya mapenzi bila ridhaa yake.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Ilenza, Halima Mohamed alisema aliamtilia shaka mwanafunzi huyo alipofika shuleni mapema asubuhi badala ya jioni ya siku iliyopita aliyotakiwa kuripoti; ndipo alipoamua kumhoji na kugundua kilichofanyika.

"Kwao mwanafunzi huyo ni Wilaya ya Magu na alitakiwa kuripoti shuleni jioni ya siku iliyopita; sasa kwa mshangao alifika shuleni asubuhi. Tulipombana akesema ukweli alipolala ndiyo tukafuatia na tukakuta bei lake kwenye chumba cha kinyozi ambaye alikiri kulala na mwanafunzi huyo,” alisema Mkuu huyo wa shule

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga alisema tayari vyombo vya dola vimechukua hatua za awali ikiwemo kumshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top