KIONGOZI WA UVCCM ATIWA NGEU KWA JAGI NA KIONGOZI WA UMOJA WA WANAWAKE CCM 'UWT' WIVU WA MAPENZI KWA MAMA LISHE

0

 Ni mshangao, ndivyo unavyoweza kueleza mkasa uliompata mmoja wa viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilayani Chemba Mkoa wa Dodoma, kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na kiongozi wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) katika mgogoro unaodaiwa kuwa wa mapenzi.

Tangu juzi zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa wilaya kupasuliwa ngeu na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa wilaya hiyo.

Taarifa hiyo, imesema kuwa kiongozi wa kiongozi huyo wa UWT kumfuata kiongozi mwenzake katika kibanda cha Mama lishe na kisha kumpiga kwa kutumia jagi la kioo ambalo lilimpasua sehemu kubwa ya kichwa.


Taarifa zinaeleza kuwa alipokwenda Kula ni mgahawa wa mwanamke mmoja ambaye amekuwa akitiliwa shaka na kiongozi huyo wa UWT anayedaiwa kuwa na uhusiano naye kimapenzi.

Taarifa hizo zinasema kuwa, kiongozi huyo wa UVCCM alifuatwa na kabla ya kupigwa ngeu, aliulizwa ni kwa nini alikwenda mahali ambapo amekuwa akizuiwa kutofika.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top