Mahakama ya makosa maalumu ya udhalilishaji Mkoa wa Kaskazini Pemba, imempeleka rumande Kombo Hamad Bakari almaarufu Kombo Arazaki kwa mwenye umri wa miaka 27, mkaazi Kambini Mchangamodogo kwa tuhuma za kumdhalilisha msichana wa miaka 15 kwa tuhuma za kutenda makosa matatu.
Kosa la kuingilia kinyume na maumbile kifungu 133(a) Sheria ya adhabu nambari 6 ya mwaka 2018.
Ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa Serikali Juma Ali Juma, mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Ali Abdul-rahman Ali, kuwa siku tarehe 03.09.2022 majira ya saa 1:00 za usiku huko Kambini Mchangamdogo Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mshitakiwa alimuingilia kinyume na maumbile msichana wa miaka 15 anayesoma darasa la sita ikiwa ni shitaka la kwanza.
Kosa
la kutorosha msichana kifungu 133(a) Sheria nambari 6 ya mwaka 2018, na kosa la kuingilia kinyume na maumbile
Aidha, katika shitaka jengine, siku ya tarehe 12.09.2022 majira ya saa 1:15 za usiku Mshitakiwa alimtorosha msichana huyo kutoka nyumbani kwao na kumpeleka anakoishi na kisha kumuingilia kinyume na maumbile jambo ambalo ni kosa kisheria.
Mshitakiwa
alikana kutenda makosa hayo na mahakama kumuamuru kwenda rumande hadi
17.10.2022 kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa ushahidi.