MAHAKAMA YAMPA SIKU 14 MAKONDA KUFIKA MAHAKAMANI

0

 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempa siku 14 aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwasilisha utetezi wake Mahakamani hapo katika kesi ya tuhuma za uporaji wa gari aina ya Range Rover.


Katika kesi hiyo, mbali na Makonda mwengine anayetuhumiwa William Malecela maarufu ‘Lemutuz’ ambapo wamefungiliwa kesi hiyo na Mfanyabiashara Patrick Christopher Kamwelwe.

Kesi hiyo imetajwa leo mbele ya Hakimu Mkazi, Richard Kabate ambaye ametoa siku 14 kwa Upande wa Mdaiwa (Makonda) kuwasilisha utetezi wake ambapo hata hivyo Makonda hakuwepo Mahakamani bali aliwakilishwa na Wakili wake Chima Andrew.
Katika kesi hiyo, Mfanyabiashara Kamwelwe anataka alipwe fidia ya zaidi ya Sh. milioni 240 ambazo ni gharama za kodi na thamani ya gari hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top