MAJAMBAZI WAVAMIA KANISA, WAPORA MALI NA KUMUUA PASTA

0

 

Kundi la Wakristu waliokuwa wamekusanyika kusali katika eneo la Diepsloot, Afrika Kusini waligeuka kuwa waathiriwa wa wizi wa kimabavu baada ya majambazi kuwavamia na kumuua Mchungaji wao.

Kulingana na ripoti, waumini wawili walijeruhiwa vibaya wakati wa kisa hicho cha kutamausha.

 News24 inaripoti kuwa kisa hicho kilitokea muda mfupi kabla ya saa usiku. 

Ripoti zinaonyesha kuwa Wakristu 50 walikuwa wamekusanyika katika kanisa lao kwa ajili ya maombi na kukesha wakati majambazi hao wenye silaha walipowashambulia.

Inasemekana kuwa majangili hao walitoroka na mali zao za thamani kama vile simu na pesa taslimu.

 Watu watatu akiwemo mchungaji walipigwa risasi wakati wa shambulio hilo na kukimbizwa kwenye kituo cha afya cha karibu, lakini mchungaji alifariki dunia alipofika hospitalini. 

Msemaji wa polisi wa Diepsloot, Luteni Kanali Mavela Masondo alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa msako wa kuwasaka wahalifu hao umeanzishwa. 

Vile vile aliongeza kuwa kesi za mauaji na jaribio la kuua zimefunguliwa. "Watu watatu waliopigwa risasi, akiwemo mchungaji, walipelekwa katika kituo cha matibabu cha eneo hilo ambapo pasta alifariki alipofika. Wengine wawili wako katika hali mbaya lakini inaendelea vizuri."
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top