MAKETE; WAZAZI WANATUAMBIA TUFELI TUKIFAULU WATAKUFA ...

0

 

Wakati serikali na wadau wa elimu wakiendelea kuboresha sekta hiyo ili iwe na tija kwa taifa, wilayani Makete mkoani Njombe imebainika kuwepo kwa baadhi ya wazazi kuwataka watoto wao wanaohitimu elimu ya msingi kufanya vibaya mtihani ili wafeli

 

Siri hiyo imefichuliwa na wanafunzi hao baada ya kuhojiwa kutokana na mabadiliko yao ya kitaaluma kuelekea wakati wa kufanya mtihani wao wa mwisho ambapo wengine wameeleza kwamba wanashinikizwa kufanya vibaya kwa kuhofia kuwapoteza wazazi wao waliowaambia kwamba wakifanya vizuri na wakafaulu, basi wazazi hao watakufa

 

Suala hilo limejitokeza katika kata ya Lupila ambapo Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Bi. Tumwanukye Ngakonda katika mahojiano na Edmo Blog na Edmo TV amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya wanafunzi kujifelisha kutokana na kusongwa na wazazi kwa kigezo kwamba wakifaulu watashindwa kuwasomesha kutokana na uchumi mgumu

 

Amesema changamoto hiyo imejitokeza baada ya Wilaya ya Makete kujiwekea na kusimamia ipasavyo mikakati ya kuhakikisha kila mwanafunzi aliyefaulu anaripoti shuleni na kuendelea na masomo ya sekondari, hivyo baada ya kusimamia vizuri mikakati hiyo ndipo wazazi wakabuni mbinu ya kuona ili wasisumbuliwe basi ni kuwarubuni watoto wao wafeli mitihani


Mtendaji Ngakonda amesema baada ya kugundua uwepo wa tatizo hilo, wamechukua hatua ikiwemo kutoa elimu kwa wanafunzi kutokubali kufeli ambapo katika utoaji elimu huo ndipo wanakutana na shuhuda mbalimbali ikiwemo wazazi kuwaambia watoto wao kuwa wakifaulu basi watafariki dunia au hawatakuwa watoto wao

Tazama video hiyo mwanzo mwisho hapa chini:-

 

Amewaomba wafanyabiashara na wadau wengine wa maendeleo kutokubali kuwa sehemu ya kuwatorosha wanafunzi kwa kigezo cha kwenda kuwapa ajira na badala yake waungane kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu kwanza

Naye Afisa Elimu Kata ya Lupila Mwl. Gabriel Sanga amemuagiza Mkuu wa shule ya sekondari Lupila kufanya tathmini kwa kila kijiji cha kata hiyo wanafunzi wangapi walianza kidato cha kwanza na wangapi wamehitimu kidato cha nne, wangapi wamejiunga na kuhitimu kidato cha sita na kwenda chuo kikuu ili wadau wa elimu wafahamu hali ilivyo, na kama mambo hayaendi waone chakufanya kwa sababu kata hiyo ni yao wote hivyo hawategemei kuona kijiji kimoja kiwe na wasomi na vijiji vingine kukosa wasomi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top