Mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Rahma Thabit Hemedi mwenye umri wa miaka 20, mkaazi wa Muembe Makumbi Mjini Unguja, amekuwa na tabia ya kuitelekeza familia yake ya watoto wanne (4) ikiwemo mtoto wake mchanga wa wiki tatu, jambo ambalo limezusha taharuki kwa familia na majirani wa mama huyo.
Akizungumza na kinasa sauti cha Mawio mama mzazi
wa mwanamke huyo, amesema kuwa kawaida humshauri mama wa watoto hao kurudi
mapema kwenye shughuli zake ili aweze kuishughulikia familia yake, lakini mama
huyo ameshindwa kuufanyia kazi ushauri huo.
“Mie humwambia kama mtoto unamuacha urudi mapema
kama vile saa 9, saa 10 lakini tangu hapo zamani anamuacha anakwenda kwenye pirika zake ambazo
sizijui hua naambiwa tu anakwenda Intebe, anakwenda Messi, Madisco disco sasa
harudi mapema na kipindi hichi cha katika kati ndio haruuuudi kitoto kianlia na
chakumfanya hatuna” alisema mama wa mwanamke huyu
Kwa upande wa majirani wa mama huyo, wamesema
inapofika saa 11 za jioni mama huyo huondoka na kurudi saa 11 za jioni ya siku
ya pili na kumnyonyesha mtoto na kuondoka tena na baadhi ya siku nyengine
anashindwa kurudi.
“Kitoto anakiacha kinalia kina wiki tatu kinapewa
uji wa sembe binafsi yangu mimi natoka na kwenda kumkosha mtoto kazi yake kwenda Intebe na
huyu ni mtoto wake wanne” Alisema mmoja wa majirani hao
Nae, sheha wa shehia hiyo Zubeir Othman, amekiri
kuwepo kwa suala hilo na kusema kitendo ni udhalilishaji wa watoto na kudai kuwa
mama huyo amekuwa na tabia hiyo ya kuitelekeza familia yake na kwenda sehemu za
starehe kwa muda mrefu.
“Huu naweza kusema kama ni udhalilishaji wa
watoto na huyu mtoto kusema ukweli ni shida mama mtu anatembea na ujusi
ukiangalia hii familia yote kusema ukweli imeoza” Sheha wa Shehia ya Muembe
Makumbi
Juhudi za Mawio za kumpata mama mzazi wa watoto
hao zimegonga mwamba kutokana kutokujuiliakana alipo mama huy.
Chanzo. Kipindi
cha Mawio