MAMA AMUUNGUZA MWANAE MIKONO KWA KUIBA TSH 250

0

 Mwanamke aitwaye Somoe Mohamed, mkazi wa kijiji cha Namanjele, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, amemuunguza vidole mtoto wake wa miaka Mitano, akimtuhumu kuiba hela shilingi Miambili na Hamsini.


Mwanamke huyo anadai mtoto wake alianza kudokoa shilingi Hamsini siku ya kwanza, kabla ya kudokoa shilingi Miambili siku iliyofuata na kisha kudokoa Dagaa, ndipo akaamua kumuunguza kwa moto vidole vya mikono.

“Nikachukua nyasi nikamvirigia mikononi nikamchoma moto…haikua kusudio langu kumchoma moto na dhamira yangu haikua hivi.” Somoe Mohamed.
 Somoe Mohamed mama wa mtoto

Baba wa mtoto huyo, Juma Lubega amesema kuwa yeye alisikia kuwa mwanaye amechomwa moto na mama ake hakuamini lakini alipofika nyumbani alimuona mtoto akiwa ameungua sehemu ya mikono yake vikiwemo vidole.

“Nilisikia uchungu kama baba nilipouliza nikaamibiwa kuwa kaiba Sh250 na kudokoa dagaa, yaani inaonyesha kuwa alimfunga kamba mikononi akaweka nyasi akamchoma mtoto na inaonyesha alipowasha moto aliondoka ndio maana mtoto amepata madhara makubwa,” amesema Lubega.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mussa Mkadimba amesema kuwa tukio hilo sio zuri kwakuwa halifundishi mtoto bali linaweza kumfanya akawa katili.

“Nimelipokea vibaya hili jambo kwakuwa halikuletwa kwangu nilisikia niliamua kulifatilia mwenyewe ili kuona kuna ukweli kiasi gani nikakuta ni kweli mtoto ameunguzwa na moto kwa maeneo ya mikoa yake.

“Huyu mtoto tangia uchomwe hajapelekwa pelekwa hosptiali yoyote wala hapata dawa zaidi ya miti shamba wanayotumia kumuwekea mikononi kutookana na imaini kuwa atapona kwakutumia dawa za asili,” amesema.

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo alipoulizwa na mwananchi kuhusu tukio hilo alisema kuwa yuko safarini na akifika atalifatilia na kulitolea maelezo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top