MASANJA ASISITIZA HATA WASEMAJE HAWEZI KUMUACHA MKEWE....KIFO KITUTENGANISHE

0

 

Mchungaji wa kanisa la Feel Free Church Emmanuel Mgaya maarufu kwa jina la Masanja Mkandamizaji amesema "Hata nikimkuta mtu anapiga game na mke wangu, namshika mkono mke wangu na kuondoka naye"


Mchekeshaji na mchungaji Masanja Mkandamizaji akiwa kanisani kwake Jumanne hii amefunguka juu ya tuhuma za mke wake kuchepuka na katibu wake ambaye amejiua kwa kujinyonga kwa mujibu wa taarifa za Jeshi la Polisi, na kusema anampenda mke wake na wale wanaotarajia kusikia kuwa wataachana wasahau, kwani hana mpango wa kumuacha mke wake huyo aliyedai ni binti mzuri.

Wiki jana pamoja pia na wiki huu skendo ya kujiua kwa katibu wa kanisa la Masanja Mkandamizaji liitwalo Feel Free imekuwa ikihusishwa kwamba alikuwa anatoka kimapenzi na mke wa baba mchungaji ambaye ni Mkandamizaji.

Masanja akizungumza na waumini wake katika video ambayo imesambazwa mitandaoni amewahakikishia kwamba yeye hayuko tayari kumwaacha mkewe leo, kesho wala akhera, liwake jua, inye mvua!

Mchungaji huyo alitokea mfano kuwa hata kama ndoa zote zilikuwa zinaisha leo hii halafu tena kesho Mungu akatoa kibali cha watu kufanya ndoa upya basi yeye atamrukia mke wake huyo huyo ambaye anazungulukwa na skendo ya kutoka kimapenzi na katibu aliyejiuwa kutokana na kile kilisemekana kuwa wivu wa kimapenzi.

Aidha wengine waling’aka kuwa katibu huyo alijiua kwa kukataliwa kimapenzi na mke wa mchungaji, na hata kuacha barua ndefu akijitoa kwa hali na mali jinsi alivyokuwa anampenda Monica, mke wa mchungaji Masanja Mkandamizaji.

Katika tamko ambalo sasa limekuwa gumzo, Masanja Mkandamizaji aliwaambia waumini wa kanisa lake kuwa hata ikatokea amemfumania mkewe moja kwa moja na mwanaume mwingine wakishiriki mapenzi, hawezi kumpiga hata kidogo bali atamshika mkono na kumutizama jamaa yule, akiona hatommudu kwa nguvu basi atamshika mkewe na kuondoka naye.

“Kwa mfano mimi sio mchungaji wala hakuna kanisa linahusika, na nimemkuta huyu dada akiwa kama mke wangu, moja kwa moja anakula uroda na jamaa. Namkamata kwanza mke wangu kwa mkono halafu nampima yule jamaa; nammudu au simmudu. Nikiona hii ngoma siiwezi kuimudu atanipasua, ninaondoka na mke wangu. Sisi tumeoana mpaka kitutenganishe kifo,” mchungaji Masanja Mkandamizaji alisema huku umati wa waumini ukipasuka kwa vicheko.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top