Mwanamke Mmoja anajulikana kwa jina la Mariamu Alex mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa kijiji ca Nkungungu Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma amedaiwa kuuwawa na mwanaume aliyekuwa akiishi naye kisha kujaribu kuuchoma moto , kuufukia na baadae kushindwa akaufunika na mifuko na kuweka matofali juu yake na kutokomea kusikojulikana.
Wakizungumzia tukio hilo mama Mzazi wa Mariamu Bi Celina John Pamoja na Mdogo wa Marehemu Michael Thomas wamesema tukio hilo lililotokea usiku wa octoba 13 katika Kijiji cha Nkungungu Wilayani Bahi huku wakidai Ugomvi wa marehemu na huyo mwanaume umekuwa ni wa muda mrefu hadi kufikia umauti.
Jitihada za kupata Jeshi la Polisi kuzungumzia tukio hili zinaendelea ili upata taarifa za mtuhumiwa wa mauwaji hayo.
CHANZO;NGASA TV